Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
……………………………………………………………………………………..
Na John Stephen
Kamati ya Afya ya Bunge leo imeitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kukagua huduma mbalimbali za afya zinazotolewa na hospitali hiyo.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Joseph Serukamba akiwamo Mussa Azzan Zungu na wabunge wengine wa kamati hiyo.
Wabunge hao wametembelea Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Idara ya Magonjwa ya Akili, Idara ya Mionzi na Wodi ya Mwaisela na chumba cha kuchakacha gesi ambayo inatumika wakati wa kutoa tiba kwa wagonjwa mbalimbali.
Daktari wa magonjwa ya Dharura na Ajali, Upendo Ndara amewaeleza wabunge hao jinsi madaktari na wauguzi wanavyowahudumia wagonjwa wanaofikishwa kwenye idara hiyo, changamoto na jinsi wanavyofanikiwa kuokoa maisha ya wagonjwa wa ajali na wagonjwa wengine.
Pia, Dk Upendo ameelezea juhudi kubwa zinazofanywa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) katika kupanua jengo la idara hiyo ili kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa.
Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Frank Massawe amewaeleza wabunge mafanikio yaliopatikana baada ya wagonjwa wa akili kupatiwa matibabu na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.
Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Frank Massawe amewaeleza wabunge mafanikio yaliopatikana baada ya wagonjwa wa akili kupatiwa matibabu na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment