Monday, April 4, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAILA ODINGA CHATO MKOANI GEITA

1Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita. Odinga alifika Chato juzi akiwa na familia yake kwa ajili ya kumpongeza Mhe. Rais pamoja na kushiriki pamoja Ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Bi. Ida Odinga.

2Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita.
3Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga, Bi Ida Odinga katika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita.
4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Raila Odiga, Ida Odinga pamoja na Mkewe mama Janeth Magufuli katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita.
5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuashiria kuagana na wageni wake, Raila Odinga pamoja na Mkewe Ida Odinga waliofika Chato juzi kwa ajili ya mapumziko na kumpongeza Mhe. Rais.
6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia watoto aliwakuta kwenye uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………………….
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga amerejea nchini Kenya baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu huko Lubambangwe katika Kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita, alikomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyepo mapumzikoni.
Akizungumza katika uwanja wa michezo wa shule ya Sekondari ya Chato kabla ya kuruka kwa Helkopta, Mheshimiwa Odinga amemshukuru rafiki yake Rais Magufuli kwa kumpokea na pia amewashukuru wananchi wa Chato kwa ukarimu wao kwa wageni.
Mheshimiwa Odinga pia amesema ana imani kuwa Rais Magufuli ataisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo umasikini unawakabili wananchi wake.
“Lakini mimi najua yeye mwenyewe ana maono, anaona mbele na anajua yale ambayo yanatakiwa yafanyike ili Tanzania iinuke, itoke katika hali ya ufukara na kuwa katika hali ya maendeleo zaidi” Amesema Mheshimiwa Odinga.
Mheshimiwa Raila Amolo Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga waliwasili Chato tarehe 02 April, 2016 kwa mapumziko na kuisalimia familia ya Rais Magufuli ambayo ni familia rafiki.
Katika Hatua nyingine Rais Magufuli ameahidi kutoa madawati na vitabu kwa wanafunzi wa shule tatu za Msingi zilizopo Chato, ambao walijitokeza katika uwanja wa Sekondari wa Chato, wakati Rais Magufuli akimuaga mgeni wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga.
Shule hizo ni Chato, Kalema na Kitela.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016

No comments: