Na Mwandishi wetu,Masasi.
KESI ya kupinga matokeo ya ubunge wajimbo la Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema )imeendelea kusogezwa baada ya mahakama kuruhusu upande wa wajibu maombi kupeleka mashahidi.
Upande wa wajibu maombi hayo umeieleza mahakama ina mashahidi mawili baada ya mahakama kuwauliza hapo jana kama watapeleka mashahidi pindi itakapotoa maamuzi kama kuna kesi ya kujibu ama la.
Kesi hiyo inayosikilizwa na jaji,Winfrida Kosoro ilitegemewa kutolewa maamuzi jana kama mjibu maombi ana kesi ya kujibu ama hana baada ya hapo jana kuwapa muda wajibu maombi kueleza kama watapeleka ama hawatapeleka mashahidi pindi mahakama itakapotoa maamuzi juu ya shauri lao la kupinga hakuna kesi ya kujibu.
Mh Tundu Lisu Akiwafafanulia jambo wananchi waliofika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo |
Mwambe alifunguliwa kesi ya kupingwa kwa matokeo na aliyekuwa mgombea mwenzake wa ubunge wa jimbo hilo Oktoba 2015,na aliyekuwa mgombea wa CCM,Mariam Kasembe.
Katika kesi hiyo ilikuwa na aya tatu ambapo mpeleka maombi alidai kulikuwa na mapungufu mengi katika mchakato mzima wa kampeni na kupinga uhalali wa matokeo hayo jambo ambalo liliwekewa pingamizi na upande wa wajibu maombi unaowakilishwa na wakili msomi, Tundu Lissu
Katika kesi hiyo mpeleka maombi aliiomba mahakama itoe tamko uchaguzi wa jimbo hilo ni batili kwasababu haukuwa huru na haki,pia aliomba mahakamakutoa amri ya kwamba uchaguzi urudiwe na kuomba gharama za kesi nzima pia anaomba kitu chochote ambacho mahakama itatoa.
Hata hivyo jaji Kosoro alisema ieleweke wazi katika sehemu ya awali ya kesi hiyo mahakama iliweza kutupilia mbali aya mbili za madai ya mlalamikaji baada ya kuona hazina mashiko.
"Ieleweke wazi katika sehemu ya awali ya kesi hii mahakama iliweza kutupilia mbili aya mbili za madai ya mlalamikaji ambayo ni sehemu ya 10a (ii) na 10B (ii) ikiona hazina mashiko,"alisema Jaji Koroso
Wa kwanza kushoto ni mjibu maombi ambaye ni mbunge wa ndanda Kupitia CHADEMA,wa tatu ni mjibu maombi wa pili mwenyekiti wa maadili uchaguzi jimbo la ndanda ambaye ni mkurugenzi wa wilaya ya masasi Beatrice Domonick |
No comments:
Post a Comment