Saturday, May 28, 2016

SONGAS WAUNGA MKONO JITIHADA ZA ELIMU NCHINI,WAKABIDHI MADAWATI 150 TEMEKE






Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia mjema amepongeza hatua ya kampuni ya umeme ya Songas kutoa msaada wa  madawati 150  ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika shughuli za kijamii pamoja na kuunga mkono agizo la Rais  wa Jamhuri ya muungano wa Tanazania Dkt John Magufuli ya kusimamia sera yake ya elimu bure katika shule ya msingi mbande.


Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo,Mbagala  juzi shuleni  hapo mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa msaada huo wa madawati 150 kutoka kampuni ya Songas utasaidia kupunguza changamoto ya watoto wa darasa la kwanza ambalo ni ongezeko kubwa limejitokeza kwa mwaka huu baada ya Rais Dkt John Magufuli kutangaza sera yake ya elimu bure.
Alisema kuwa kuna mahitaji ya madawati takribani 29500,vyumba vya madarasa 2881 kwa wilaya hiyo ambayo yanatakiwa kujengwa ili kupunguza changamoto za wanafunzi kukosa sehemu ya kusomea pamoja na kukaa chini hivyo ni jambo jema kuiunga mkono serikali yake katika kusimamia maenedeleo ya elimu.
Hata hivyo mkuu wa wilaya huyo ameahidi kusimamia na kutekeleza agizo la Rais katika kuhakikisha wanafunzi wanapata madarasa na madawati ili kuwapa hamasa za kusoma vizuri kwa lengo la kuja kuwa viongozi bora wa kesho ambao wataipatia nchi sifa na mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

"Ndugu zangu wandegereko watoto tuwasomeshe,lazima mtoto aende shuleni kupata elimu sisi serikali tutasimamia hilo ili kila mtoto apate elimu ili kesho waje kuwa madaktari na marubani.madaktari watatutibu meno,sawa aliuzia mkuu wa wilaya huyo".
Hata hivyo Afisa Ugavi wa Manispaa ya Temeke Mashaka Kipande amesisitiza kuwa halmashauri yake ya Temeke imeelekeza nguvu za kutosha katika ujenzi wa madarasa ambapo mpaka ujenzi upo hatua ya kupaua ambayo inakaribia kuanza hivi karibuni.
"Kwa niaba ya mkurugenzi sisi kama halmashauri tumejipanga vizuri na ujenzi umefikia katika hatua ya kupaua ambayo itakamilika muda mchache ujao hivyo ifikapo mwezi ujao mradi utakuwa umekamilika"alisema.

Naye mratibu wa mahusiano ya kijamii ya kampuni ya Songos Nicodemus Chipakapaka ameahidi kutoa msaada wa ujenzi wa madarasa mawili ikiwa ni sehemu za kuhamasisha wazazi,na wadau wa maendeleo kuunga mkono jitihada hizo za kuchangia elimu. 

No comments: