Saturday, May 28, 2016

MKUU WA WILAYA TEMEKE SOPHIA MJEMA AUNGANA NA WANANCHI KUFANYA USAFI MAENEO MBALIMBALI

Mkuu wa wilaya ya Temeke SOPHIA MJEMA akiwa katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya wilaya yake ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Serikali kuwa kila Jumamosi iwe ni siku ya Usafi 
Mkuu wa wilaya ya  Temeke Sophia Mjema amesema wakazi wake  wanatakiwa kuhakikisha wanajitoa na kuhamasika katika utunzaji wa mazingira kwa kuamua kupiga vita uchafu wa mazingira sambamba na kuepuka umwagaji wa maji holela katika maeneo ya miundo mbinu hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya jamii.


Wakati huo huo Mkuu wa wilaya amekemea vikali hatua wafanyabiashara wa soko la Tandika ambao wanashindwa kutambua jukumu lao katika kuyalinda maeneo yao ya biashara kwakuyaweka mazingira hayo katika hali ya usafi.

Aidha Mkuu wa wilaya hiyo ametoa agizo kwa viongozi wa soko hilo kuhakikisha wanasimamia agizo la serikali la usafi ikwemo kulinda miundo mbinu iliyopo ndani ya soko hilo kwakuwa mifereji inayozunguka soko hilo inashindwa kutunzwa ipasavyo.

Hata hivyo Afisa afya wa manispaa ya Temeke Williamu Muhemu amesisitiza kuwa idara yake kwakushirikiana na mkuu wa wilaya watasimamia ipasavyo agizo la Rais ili Temeke iwe kivutio cha wawekezaji kwa nyakati za usoni.

"Kama ilivyo kauli ya mbiu isemayo 'Temeke ya Mjema' tupo imara katika mapambano ya usafi hivyo tunaahidi kutokomeza uchafu wilaya ya Temeke inayoongozwa na mkuu wa wilaya hodari"alisema Muhemu.

Naye Mwenyekiti wa soko la TandikaYusuph Mpina amepongeza hatua ya mkuu wa wilaya huyo kufuatia hatua ya kuamua kuanzisha operesheni yake ya usafi ya kila sehemu kawkuwa kumemabidiliko na mapokeo makubwa katika utunzaji wa mazingira mahali pakazi na majumbani.

"Nampongeza sana Mkuu wa wilaya ya Temeke mama Mjema,naunga mkono jitihada zake za kupambana na uchafu sisi kama wafanyabiashara tunaungana naye katika kuyaweka maeneo ya biashara salama,pia naomba viongozi wengine kuiga mfano wa mkuu wa wilaya yetu nayekuja kwa wananchi"alisema Shaban.

No comments: