Sunday, May 8, 2016

TREVO YAWAJAZA WATANZANIA MAHELA NA AFYA BORA

Mkurugenzi wa Bidhaa ya Trevo nchini Tanzania Bwana David Kagoro akionyesha bidhaa hizo mbele ya wanahabari waliofika katika tukio hilo
Kampuni ya Trevo imetajwa kuwa ni suluhisho katika afya ya Binadamu pamoja na kukuza uchumi wa wananchi waliojiunga na kufanya biashara tangu kampuni hiyo ilipo anzishwa nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa  Mkurugenzi  wa  Kampuni  ya  Trevo  nchini  Tanzania Bw. David Kagoro amesema Kampuni  ya Trevo ambayo ina miezi 17 hivisasa nchini Tanzania imeweza kutoa kwa wananchi kiasi shilingi za kitanzania bilioni tatu na nusu ambazo ni ujira wao kutokana na mauzo waliyoyafanya kupitia biashara kwa njia ya mtandao (Network Marketing)..
Mkurugenzi huyo amesema tayari hadi sasa watu wanne wamepata fulsa ya kupata magari mapya wakiwa ni watanzania katika kipindi cha mwanzo ambapo biashara ya Trevo bado ilikuwa haijafahamika.
Ameongeza kuwa katika sherehe ya ‘Elevate’  wananchi waliojiunga na kufanya biashara na Trevo wamepata zawadi za aina mbalimbali zikiwemo  fedha, Gari, Tuzo mbalimbali.
Bw, Kagoro amesema Mwezi ujao watakuwa jijini Mbeya na Mwezi julai watafanya tena sherehe ya Elavate jijini Dar es salaam.
Rais wa Trevo Mark Stevens katikati akizngumza na wanahabari kuhusu mipango mbalimbali na Jinsi watanzania walivyonufaika na Trevo pembeni ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trevo nchini Tanzania Bw. David Kagoro (kushoto).
Kwa upande wake Rais wa Trevo Mark Stevens amesema kwamba Kampuni ya Trevo imewapa fursa vijana wa kitanzania kuvuna fedha kutokana na juhudi zao kwa kuwa Biashara ya Trevo imeshamiri nchini na inaendelea kukita mizizi katika maeneo mbalimbali.

Amesema bidhaa ya Trevo ni maarufu duniani kote kwani  ina mchanganyiko wa matunda aina 174 ambayo kwa pamoja yanasaidia katika kuboresha afya ya mtumiaji.
Hadi sasa kampuni ya Trevo ina ofisi tatu zilizopo Dar es salaam, Mbeya na Arusha pamoja na vituo vya kuchukulia mzigo 15 nchi nzima.
Vituo hivyo  vipo  katika maeneo ya Mwanza, Bukoba,Geita,Singida, Babati, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Songea, Zanzibar na sehemu nyingine.




No comments: