Baada ya chama cha
ALIANCE FOR DEMOCTARIC CHANGE –ADC kuingia
katika migogoro ya kiuongozi ndani ya chama hicho siku za hivi karibuni Hatimaye
hali ya Amani imerejea ambapo chama hicho leo kimeingia katika mkutano mkuu
uliowakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka kila kona ya nchi.
Katika mkutano ambao
umehudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo waziri wa kilimo wa
serikali ya Zanzibar ambaye alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
chama hicho ambaye pia ndiye mlezi wa chama Mh HAMAD Rashid,viongozi kutoka ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa na wajumbe mbalimbali wa chama hicho.
Makamu mwenyekiti wa ADC Mama ADELA STOLIC akihutubia wakati akifungua mkutano huo Mkuu mapema leo |
Akizngumza wakati wa
Ufunguzi wa mkutano huo HAMAD RASHID amesema kuwa chama cha ADC ni chama
ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia watanzania,kikiwa na itikadi
zake,sera zake na mipango yake hivyo hakipo tayari kufwata sera za chama
kingine chochote nchini na swala la kushiriki chaguzi mbalimbali ni moja kati
ya sera zao hivyo hawapo tayari kususia uchaguzi wa aina yoyote kwani ndio njia
pekee ya kupata viongozi wa nchi.
Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini A SISTY LEORNAD NYAHOZI akitoa hotuba fupi kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa nchini |
Ameleza kuwa chama
chake kimeanza mipango kabambe ya kujiimarisha Zaidi kwa lengo la kuwaletea
mabadiliko ya kweli watanzania baada ya wapinzani wao waliokuwa wakiongoza
serikali iliyopita na sasa hawapo kushindwa kufanya hivyo kwa miaka yote
iliyopita hivyo amewataka watanzania kuanza kukiamini chama cha ADC kwani ndio
dira pekee ya mabadiliko kwa watanzania kwa sasa.
Akizungumzia kuhusu
upatikanaji wa viongozi wa chama hicho mara baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa
mwenyekiti wa chama kiongozi huyo amewataka wanachama wa chama hicho wakae
tayari kwa kuwa siku yoyote chama kitaitisha uchaguzi wa kupata viongozi wapya.
Naye msajili msaidizi
wa vyama vya siasa nchini Mh SISTY LEORNAD NYAHOZI akizungumza katika mkutano
huo amekipongeza chama hicho kwa kukubali kuingia katika uchaguzi wa marudio
Visiwani Zanzibar ambapo walishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 3 jambo
ambalo amesema ni ukomavu wa kisiasa kwa chama kichanga kama hicho kushiriki
uchaguzi mkubwa kama ule na kupata mafanikio hayo.
Aidha amesema kuwa
chama hicho kimeonyesha ukomavu Zaidi baada ya kutokea mtafaruku na aliyekuwa
mwenyekiti wa chama hicho na kufanikiwa kulimaliza kidemocrasia jambo ambalo
amesema linafaa kuigwa na vyama vingine vya siasa nchini.
Chama hicho kilijikuta
katika migogoro iliyosababisha hadi kutimuliwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wake
SAID MIRAAJ kwa kile kiliichoitwa kukiuka matakwa katiba ya chama ambapo
ilielezwa kuwa mwenyekiti huyo alipinga kitendo cha viongozi wa chama kuingia katika uchaguzi wa Zanzibar wa marudio
jambo ambalo alilipinga na kusababisha mtafaruku baina yake na aliyekuwa
mgombea wa chama hicho visiwani Zanzibar ambaye kwa sasa ni waziri HAMAD
RASHID.
No comments:
Post a Comment