ULISIKIA SAKATA LA WAMACHINGA KUTAKIWA KUHAMA KARIAKOO,SASA LEO WAMEIBUKA NA KUPINGA,IPO HAPA
Siku
moja imepita tangu Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Isaya Mnguruni kutoa tamko kuwa
wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga wanatakiwa waondoke
maeneo ya Kariakoo mpaka kufikia siku ya jumamosi na kwenda maeneo
waliyo pangiwa kwa madai ya kuwa sehemu hizo zimekidhi vigezo vya wao
kufanya biashara.
Tamko
hilo limepokelewa tofauti na Machinga ambapo Mwenyekiti wa
wafanyabiashara ndogondogo katika Halmashauri ya Ilala Steven Lusinde
ameeleza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo waliamua kutembelea maeneo
hayo ambayo ni Ukonga,Tabata Muslim,Kigogo Fresh,Kivule na kukuta hayapo
katika miundombinu stahiki, yakikabiliwa na changamoto mbalimbali.
Akizitaja
baadhi ya changamoto hizo Lusinde amesema wamekuta maeneo yamevamiwa na
watu wanaojiita wazawa hivyo wakienda huko wanahofu ya kutokea uvunjifu
wa amani, huku mengine yakiwa hayana vizimba, huduma ya choo na maji.
Lusinde
ameongeza kuwa hawapingani na serikali kuhusu wao kuondoka ila ni vyema
serikali ikajipanga kwa kuboresha mazingira na kutatua migogoro
iliyopo, kwani bila kufanya hivyo watakuwa hawawatendei haki.
No comments:
Post a Comment