Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD akiwa anabadilishana mkataba na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini ;LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA baada ya kusaini mkataba mpya wa mashirikiano baina ya nchi ya Norway na LHRC mkataba ambao utadumu kwa miaka mitatu zaidi.PICHA NA EXAUD MSAKA HABARI |
Balozi wa wa Norway nchini
Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD amekimwagia sifa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu Nchini Tanzania LHRC kwa juhudi kubwa wanazozionyesha katika
kuwasaidia watanzania kuwatetea kupata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na
kuwasaidia watu kisheria.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD akiwa anasaini mkataba huo pembeni ni Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini ;LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA naye akisaini kuashiria kukua kwa ushirikiano wao |
Kauli hiyo ameitoa leo
Jijini Dar es salaam alipotembelea kituo hicho chenye maskani yake Kijitonyama
na kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu zaidi wa mashirikiano Baina ya nchi
yake na Kituo hicho mkataba ambao umetajwa kuwa utawezesha wanaharakati hao
kuendelea kupigania haki za watanzania kwa hari mpya.
HANNE akizungumza na
wanahabari ambao walifika kushughudia tendo hilo la kusaini mkata mpya amesema
kuwa Nchi ya NORWAY wamekuwa wakiwaunga mkono LHRC tangu mwaka 2004 ambapo
amekiri kuwa tangu waanze kutoa ufadhili kwa wanaharakati hao wamekuwa wakiona
mambo makubwa wanayofanya na hawajuti kuwa wabia wa kituo hicho.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini ;LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizngumza na wanahabari baada ya kusaini mkataba huo |
Ameongeza kuwa wakati
kituo hicho cha sheria na haki za binadamu kikiwa kimetimiza miaka 20 ya uwepo
wake mwaka jana kimeonekana kuwa ndio shirika bora na imara la kutetea haki za
binadamu nchini Tanzania jambo ambalo amesema linafaa kupongezwa na kila
mtanzania ambaye anatetea haki za watu na kuahidi kuendelea kuwa nao pamoja ili
kufanikisha malengo ambayo wamejiwekea.
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi HANNE MARIE KAARSTAD akizungumza na wanahabari waliofika kushughudia Tendo hilo. |
Aidha amesema kuwa nchi
yake imekuwa ni moja kati ya nchi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kushirikiana
na mashirika ya kimataifa ambayo yanapigania haki za wanadamu jambo ambalo
liliwapa nguvu ya kuanzisha mashirikiano na LHRC kwa kuwa wanachokifanya ni
jambo jema ambalo linafaa kuungwa mkono na kila mtu.
Akizungumza katika
hafla hiyo Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA pamoja na
kushukuru kwa ujio wa Balozi huyo na mkataba huo amesema kuwa mkataba huo mpya
utawasaidia katika kuendeleza mapambano ya kupigania haki na kufikia malengo
waliojiwekea ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kisheria maeneo
mbalimbali,kuhamasisha watanzania kuzitambua haki zao na shughuli nyingine
ambazo zinafanywa na kituo hicho.
Mkataba huo unatajwa
kufikia pesa za Norway Prona million 17.
No comments:
Post a Comment