KAMPUNI ya Hope Light Film inayojishughulisha na uandaaji wa filamu,Documenti na shughuli mbalimbali ambazo zinawiana na uchukuaji wa picha za mnato na video imeunda group ambalo litaweka ukaribu baina ya wadau na mashabiki wa filamu za Bongo Movie katika kujadiliana mambo mbalimbali katika uendelezaji wa kazi za sanaa nchini.
Akitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook,Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Ally Njenje,alisema kuwa ameunda kundi la ALLY NJENJE FANS kupitia Whatsap na Facebook ili kuwaleta pamoja wadau na mashabiki wa kazi za filamu za bongo movie za hapa nchini pamoja na kuunganisha katika mzunguko wa biashara kwa wao kama hope Light Film kutangaza kazi zao na kwa watu wengine pia kutangaza biashara zao ambapo linakuwa kundi la kubadilishana mawazo ya kujiinua kiuchumi lakini pia kusapotiana katika suala zima la biashara.
“Ndugu zangu wadau wa Kampuni ya Hope Light Film napenda kuwajuza kuwa nimeunda group la ALLY NJENJE FANS ambalo linaweka karibu mashabiki wa kazi zetu na kwa sababu wewe ni shabiki wangu nami pia ni shabiki wako ambapo katika kundi hili ni vyema kila mtu ajitambulishe kwa kazi anayofanya ili tupeane fursa wenyewe kwa wenyewe kwa mfano nikijua wewe unafanya biashara aina fulani basi humu kaa ukijua kuna wateja wako mmoja wapo ni mimi Ally Njenje lakini isiwe biashara hatarishi”Alisema Njenje
Aidha amesema kuwa watu wote watakaojiunga na kundi hilo watapata fursa ya kuwa wa kwanza kuangalia kazi za Hope Light Film na kwa wale wote watakaokuwa tayari kuisambaza kwenye libraly zao au zilizokuwa karibu yao au kwa wateja wowote wale na kwa mwanakundi yeyote atakayekuwa tayari kuchukua copy kadhaa ambazo ataenda kuziuza kwa kila copy atakayouza kutakuwa na pesa yake ni mwanakikundi na uwezo wake wa uchakarikaji katika uuzaji wa kazi hizo.
“Ndio maana nasema kuwa ukiwa ndani ya kundi hili utakuwa wa kwanza kuona kazi zangu na kazi za Hope Light Film ili uangalie uzuri wake na kuangalia wapi utapeleka kuuza kazi hizo suala hili ni la hiyari sio shuruti kwa mwenye kuiona fursa hii ya biashara ambayo itakusaidia wewe na mimi kupata faida katika kundi hili anakaribishwa sana”Alisema Njenje
Aliongeza kwa kutoa nafasi kwa mtu yeyote mwenye kuona ana kipaji na ana nia ya kushiriki katika kampuni yake kama muigizaji na akaongeza kusema kuna nafasi nyingi sana ambazo zinahitaji watu kama uandishi wa stori za filamu,upigaji wa picha za mnato na jongefu,kuongoza filamu,kuwafanyia make up waigizaji pamoja na kuwa mshauri katika uboreshaji wa utengezaji wa filamu za Hope Light Film ili kutoa kazi bora.
“Kama unahisi ndozto zako ni kuigiza na hayo niliyoainisha hapo juu ukiwa kama kijana au mtu wa rika lolote nakukaribisha kwenye group hili ili tufahamiane na kusaidiana katika kujikwamua kiuchumi na kimaisha pia nataraji siku za karibuni kuanzisha academy ya kulea watoto na watu wakubwa katika kuwajenga kisanaa kwa kuwa naamini mimi ni msaada mkubwa kwao nitajitolea kutoa elimu ya uigizaji na kuwapa nafasi wewe,kijana wako au ndugu yako aliyeunganishwa au kupata taarifa hii kupitia mtu aliyejiunga katika group langu la Ally Njenje Fans kwa sababu umenipa thamani kubwa name napaswa kukurudishia thamani hiyo”Alisema Njenje
Alimaliza kwa kutoa wito kwa watu wote wenye kuona wanaweza kuchangamkia fursa hiyo wajitokeze mapema kumtafuta kupitia mtandao wa facebook kwa jina la Ally Njenje au kwa Whatsap namba yake 0713103521 na kutoa angalizo kuwa katika kundi hilo heshima na maadili ya mtanzania yazingatiwe kwa kuwa ni katika kundi hilo kutakuwa na watu wa rika mbalimbali na kushauri watu kuacha tabia ya kufuatana inbox kuelezana mambo ya kijinga wengi wao katika kundi hilo wana ndoa zao mtu anapokuchekea haimaanishi anakutaka au anastahili kusumbuliwa mtu anapokuheshimu na yeye mheshimu.
No comments:
Post a Comment