Wednesday, June 8, 2016

HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA ZITTO AHOJIWE NA JESHI LA POLISI LEO


Kongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe amemaliza mahojiano na maofisa wa Polisi na kisha kuongea na waandishi wa habari

Ameeleza kuwa amehojiwa juu ya maombi ya mkutano uliofanyika Mbagala Zakhiem Juni 5 mwaka huu kwamba maombi yalikuwa na maudhui kujenga chama badala yake ukafanyika uzinduzi wa Operesheni Linda Demokrasia

Pia ameelezwa kuwa katika mkutano huo Zitto alimtaka Rais awaambie ukweli wananchi juu ya sakata la kuadimika kwa sukari na kwamba Rais asiwe muongeaji sana katika kila eneo kwamba "aliropoka kuhusu sukari
Pia katika mahojiano hayo ya Polisi imeelezwa kuwa wametafsiri kitendo cha Zitto kuhoji kauli ya Rais Magufuli kuwaita wanafunzi waliofukuzwa chuo Kikuu cha UDOM kuwa ni vilaza kina lengo la kumchonganisha Rais na wananchi kuhusu suala hilo

Pia Zitto amehojiwa katika mahojiano hayo juu ya kauli yake aliyomnukuu Rais akisema kuwa ni Rais wa Masikini ina lengo la kumgombanisha kiongozi wa nchi na matajiri
Na mwisho amehojiwa juu ya kuelezea daliki za udikteta na kuunasibisha uongozi wa awamu ya tano na dalili hizo za udikteta kwa kusema Rais anaendesha nchi kiimla
Hayo yote yapo chini ya kifungu 89(1)(a) cha Penal Code kwamba " ametumia maneno ya matusi yenye kuweza kuvunja Amani .



No comments: