WAKATI nchi ya Tanzania
ikiwa katika sintofahamau kubwa kutokana na matukio ya mauaji ambayo yameitikisa
nchi kwa kipindi kifupi na kuacha watanzania wakiwa katika wasiwasi mkubwa naye
kiongozi mkuu wa waislam wa dhahebu la shia nchini Tanzania Seikh HEMED JALALA
ameibuka na kulaani vikali mauaji ambayo
ameyaita ya kiigaidi yaliyotokea katika mikoa mbalimbali nchini huku akisema
kuwa vitendo hivyo vinakwenda kinyume na Imani ya dini yoyote nchini na vinastahili
kupingwa na kila mtanzania.
Akizungumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam wakati akitoa salamu za pongezi kwa
waislam wote kwa kuuanza mwezi wa mfungo wa ramadhani Sheikh JALALA amesema kuwa
Tanzania ni nchi iliyotambulika duniani kote kuwa kisiwa ya Amani na utulivu hivyo vitendo hivyo ni
vitendo ambavyo vinaharibu sifa ya nchi duniani kote.
Ameongeza kuwa vitendo
vya ugaidi na ukatili pamoja na uvunjifu wa Amani nchini ni vitu vya kuwa
makini sana na kuwa na tahadhari sana kwani vinaweza kuzuia hata waumini
mbalimbali kuabudu kwa uhuru na Amani hasa kipindi hiku cha mfungo
Aidha amewataka
watanzania sasa kuchukua jukumu la kuwa walinzi wa maeneo wanayoishi na
kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa haraka pale ambapo wanaona watu au kikundi cha
watu ambao hawaeleweki wakiwa katika maeneo yao huku akivitaka vyombo vya
usalama kuhakikisha kuwa wanachukua taarifa za wananchi na kuzifanyia kazi mara
moja ili kuepuka kutokea kwa matukio ya kigaidi na mauaji kama yaliyotokea
mwezi huu.
Tukumbuke kuwa siku za
hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio ya mauaji ya kutisha huku
wengine wakichinjwa ambayo yaiyokea mkoani mwanza na mengine mkoani tanga
matukio ambayo yameacha simanzi kwa watanzania walio wengi.
Katika hatua nytingine
Sheikh JALALA akizungumzia mwezi mtukufu wa ramadhani amewataka waislam wote
nchini kuutumia mwezi huo kama mwezi wa
kuwa karibu Zaidi na mungu na kuhakikisha kuwa wanautumia kudumisha Amani na
umoja uliopo nchini.
No comments:
Post a Comment