Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
RAIS Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza Juni 28,2016 hadi Julai 8,2016 ambayo yatafunguliwa rasmi Julai 1,2016 na Rais huyo akiambatana na mwenyeji wake Rais Dk.John Magufuli.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka alisema maonesho hayo yatatoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi pamoja na taasisi mbalimbali kutangaza biashara na huduma wanazotoa, kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza jukwaa la kibishara ambap hutoa fursa kwa wafanyabiashara kutengeneza mitandao ya mawasiliano baina yao inayowasaidia kukuza biashara na kufikia malengo waliyojiwekea na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao.
Rutageruka alisema nchi 30 zitashiriki maonesho hayo huku makampuni yakiwa 650.
Alitaja viingilio katika maonesho hayo kuwa kwa watoto itakuwa ni sh.1000 na wakubwa sh.3000 hiyo ni kuanzia Juni 28n hadi Julai 8,2016 lakini katika siku ya Julai 7, 2016 kwa wakubwa itakuwa ni sh.4000.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kutembelea kwenye maonesho hayo ili kujifunza mambo ya biashara.
No comments:
Post a Comment