Saturday, June 4, 2016

STARS YA MWENDOKASI ILIVYOPIGWA NA MAFARAO LEO TAIFA

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa amekubali matokeo baad ya kufungwa goli 2 – 0 na Misri huku akisifia kikosi chao kuwa ni kizuri na wana wachezaji wazuri na wamecheza kwa nidhamu kubwa sana.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkwasa amesema wachezaji wake wamecheza vizuri ila wameshindwa kutumia nafasi walizozipata katika kipindi cha kwanza na makosa madogomadogo kutoka kwa wachezaji na hasa ukiangalia goli la pili lilikuwa ni kosa la mabeki katika kufanya marking ya mwisho. Hata hivyo nawapongeza sana Misri kwani wamepata alama tatu na kuweza kufuzu Mataifa Afrika 2017 nchini Gabon.
“Wachezaji wamejituma sana na siwezi kuwalaumu kwani wamecheza na timu yenye uwezo mkubwa sana na wana wachezaji wa kimataifa wengi wanaocheza soka la kulipwa nje,”amesema Mkwasa.Baada ya matokeo hayo Stars wamesalia na pointi moja na Misri kujiongezea alama tatu na kufikisha saba ambazo zimempa nafasi ya kufuzu AFCON.

No comments: