Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba nchini Tanzania DEUS KIBAMBA amesema kuwa mpaka sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR J.P MAGUFULI amelitaja neno KATIBA MPYA mara mbili tu jambo ambalo linaleta shaka kama serikali yake ina nia ya kufufua mchakato huo ambao uliachwa kiporo na Serikali ya awamu ya nne.
Bwana KIBAMBA aliyasema hayo mwishoni mwa wiki hii wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake juu ya harakati ambazo wamezianza tena wao kama JUKATA katika kudai katiba mpya nchini.
IPO VIDEO HAPA UNAWEZA KUTIZAMA |
No comments:
Post a Comment