Thursday, June 9, 2016

WANAFUNZI WALIOITWA VILAZA WAIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI

WAKATI serikali chini ikiwa imeshikilia kauli yake kuwa wanafunzi 480 waliofukuzwa katika chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph ni “vilaza” na hawana sifa ya kudahiliwa kwenye chuo kikuu nchini ,
Nao wanafunzi hao wameibuka na kuishtaki Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU)  mahakamani  kwa hatua ya kuwaruhusu wanafunzi hao kujiuunga na chuo kikuu wakati wakiwa hawana sifa.

 Mbali na (TCU) pia wanafunzi hao wamekishtaki Chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph kwa  hatua yake ya kuchukua ada za masomo wanafunzi hao  huku wakijua hawana sifa za kusoma chuo kikuu.

Licha kukistaki chuo hicho pia wameitaka mahakama kuzuia mara moja masomo yote yanayoendelea katika chuo hicho mpaka haki yao ya msingi itakaposikilizwa na mahakama.

Akithibitishwa kufunguliwa kwa kesi huyo,Emmanual Muga ambaye ni wakili kutoka kampuni ya Agustino Law Office amewaambia waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam,kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwenye Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam  na kupangiwa  kusikilizwa na Jaji wa mahakama hiyo Elieza Felishi.
Wakili Muga amesema kesi hiyo ya namba 311 ya mwaka 2016 inatarajiwa kuanza kutajwa kesho ambapo wanafunzi 316 kati ya 480 ya waliofukuzwa ndio wamefungua kesi wakitaka haki ya sheria ingilia kati maamuzi yaliyofanywa na Serikali.

No comments: