Thursday, June 9, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA HASHIM THABEET MCHEZAJI WA NBA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mchezaji wa kikapu wa kulipwa nchini
Marekani, Mtanzania Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar
es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake
wa  kuanzisha na kukuza michezo pamoja na vituo vya Michezo
hapa Nchini.
 Mchezaji wa kikapu wa kulipwa nchini
Marekani, Mtanzania Hashim Thabeet akisaini moja ya mpira mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan, akipokea Zawadi ya Mpira kutoka kwa Mchezaji wa Mpira wa
kulipwa wa Kikapu nchini Marekani Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa
Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu
lengo na mpango wake wa  kuanzisha na
kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa Mpira
wa kulipwa wa Kikapu nchini Marekani Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa
Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu
lengo na mpango wake wa  kuanzisha na
kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini. (PIcha na OMR)

No comments: