Na Vicent Macha-Dar es
salaam
Ikiwa Tanzania na Africa
tukiadhimisha siku ya mtoto wa Africa siku ya kukumbuka watoto Zaidi ya 300 waliouwawa
nchini Africa kusini wakiwa katika maandamano,Seriali ya Tanzania kupia Bunge
lake wametakiwa kufanya marekebiho sheria zote nchini ambazo zinamkandamiza mtoto
pamoja na kuhakikisha kuwa sheria zilizopo kuhusu mtoto zinatekelezwa kwa
umakini na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaofanyia watoto
vitendo vya ukatili.
Wito huo umetolewa leo
Jijini Dar es salaam na watoto kutoka shule mbalimbali walipokuwa wanatoa maoni
yao katika maadhimisho yaliyoandaliwa na kituo cha sheria na haki za Binadamu
nchini LHRC kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo ambapo wamesema kuwa pamoja na
kuwepo kwa sheria nyingi za kumlinda mtoto nchini lakini bado kuna sheria kandamizi
kwa motto ambazo zinahitaji mabadiliko ya haraka kwa kuwa zinazidi kuwaumiza
watoto nchini.
GLORIA SAMBO ni
mwanafunzi aliyesoma hotuba kwa niaba ya wenzake ameeleza kuwa vitendo vya
ukandamizaji nchini bado vinashamiri ambapo ametolea mfano swala la wazazi na walezi
kuwakutuma vileo watoto wao pamoja na kwenda nao katika kumbi za starehe mambo
ambayo yanahitaji kusimamiwa na serikali na sheria kuchukua mkondo wake mara
moja.
Mwanafunzi GLORIA SAMBO akisoma Hotuba ya watoto hao kwa niaba ya wenzake katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto Frica yaliyoadhimishwa na Kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini LHRC Jijini Dar es salaam |
Ametaja pia swala lingine
ni maaswala mazima ya ajira za utotoni,kutoroshwa kwenda nje ya nchi kwa ajili
ya kutumikishwa,biashara za ngono kwa watoto,watoto kushirikishwa katika biashara
za madawa ya kulevya,na kuwauwa kwa Imani za kishirikina pamoja na adhabu kali
kutoka kwa wazazi na walezi mambo ambayo yote yametajwa kuwa serikali inatakiwa
kusimamia sheria ili kuwalinda watoto na maswala hayo.
Moja kati ya sheria
ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa maswala ya haki za watoto
ni pamoja na sheria ya motto ya mwaka 2009 kwenye maswala ya ndoa ambapo
inakinzaa na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 kinachoruhusu mtoto wa
kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi na miaka 14 kwa ridhaa
ya mahakama,hali ambayo inafanya Tanzania kuwa kati nchi zenye kiwango kikubwa
cha ndoa za utotoni kwa nchi za Africa.
Akizungumza na watoto hao Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELEN KIJO BISIMBA leo katika maadhimisho hayo ya mtoto wa Africa yaliyoadhimishwa na LHRC Jijini Dar es salaam. |
Watoto hao wameitaka
serikali kuiagalia upya sheria hiyo kwani ni sheria kandamizi moja wapo katika
nchi na imekuwa ikigharimu maisha ya watoto wengi kupoteza haki zao za msingi.
Aidha katika hatua
nyingine watoto hao wametoa wito kwa watanzania kwa Ujumla kuheshimu haki za
mtoto,pamoja na makundi muhimu yenye ushawishi katika jamii wakiwemo viongozi
wa dini kuhubiri haki za watoto na kuwatahadharisha wanajamii wanaowaongoza
kuwa na hofu ya mungu ili kuepuka kutenda dhambi ikiwemo uvunjaji wa haki za
mtoto.
Akizungumza na watoto
hao Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELEN KIJO BISIMBA amesema kuwa katika
maswala ya watoto kila mtanzania anastahili kuhusika kikamilifu katika kulinda
na kuheshimu haki za mtoto na sio jukumu la mtu Fulani au serikali pekee bali
ni jukumu la watu wote.
Siku ya mtoto wa Africa
huazimishwa kote barani Africa kwa lengo la kutambua thamani utu umuhimu wa
mtoto duniani ikiwa ni kumbukumbu ya watoto 300 waliouwawa nchini Africa kusini
ambapo nchni Tanzania kauli mbiu ni kupambana na mila potofu zinazomkandamiza
mtoto na tabia zote mbaya dhidi ya mtoto.
PICHA NYINGINE ZA SHUGHULI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WATOTO HAO ZIKIWEMO MAIGIZO NA MICHEZO MBALIMBALI KAMA ISHARA YA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRICA.
No comments:
Post a Comment