Monday, June 6, 2016

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROFESA MAGEMBE AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA NA WANAHABARI WAANDAMIZI UKUMBI WA VETA MKOANI LEO

 Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Magembe akihutubia wanahabari na wadau wa sekta ya utalii wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali mjini Morogoro leo asubuhi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi, akihutubia katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wanahabari katika mkutano huo wakati akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Magembe kuhutubia.
Meneja Mawasiliano Tanapa, Pascal Shelutete akiwasomea wanahabari ratiba ya mkutano huo wa siku tatu.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakisoma ratiba ya mkutano huo.
Watoa mada mbalimbali katika mkutano huo wakiwa tayari kwa kazi hiyo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti Tafori, Felician Kilahama, Jaji wa Tuzo za Habari za TANAPA, Jack Muna, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Dk.Ayub Rioba na Profesa Wineaster Anderson kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Hapa ni kazi tu wanahabari wakiwa kazini.
Taswira ya ukumbi katika mkutano huo.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Meza kuu ilivyokuwa ikionekana katika mkutano huo.
Wahariri na waandishi wa habari wandamizi wakiwa ukumbini.
Mpiga picha Fadhili Akida kutoka magazeti ya serikali akiwa kazini ' hapana kuchezea job'

No comments: