Na Exaud Mtei
Serikali ya Tanzania imetakiwa
kufanya marekebisho makubwa ya sheria ya mirathi ya kimila sheria ambayo
imetajwa kuwa ni kandamizi na inawanyima haki wanawake na wasichana ikiwa ni
utekelezaji wa mkataba wa CEDAW ambao nchi imesaini mwaka 1986 ambapo ulikuwa
unawaelekeza wanachama kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi za
kisiasa,kiuchumi,na kijamii ili kuletwa usawa.
Wito huo umetolewa leo
jijini Dar es salaam na kikosi kazi cha kamati ya mkataba wa kuondoa aina zote
za ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW ambacho kinaundwa na mashirika tisa
yanayotetea haki za wanawake Tanzania kwa namna mbalimbali.
Akizungumza
kwa niaba ya mashirika hayo yote mkurugenzi mtendaji wa kituo cha msaada wa
kisheria kwa wanawake WLAC ambao wameyaongoza mashirika hayo katika tamko hilo
Bi Theodosia Nuhulo ameeleza kuwa mnamo mwaka 2005 WLAC kwa kushirikana na wadau wengine watetezi
wa haki za wanawake walifungua kesi mkakati katika mahakama kuu ya Tanzania
kanda ya Dar es salaam kupinga vipengele kandamizi katika sheria hiyo ya
mirathi (Tamko la Mirathi la kimila) la mwaka 1963 lakini mnamo mwaka 2006
ilitupilia mbali kesi hiyo huku ikitamka wazi kuwa vifungu vilivyolalamikiwa ni
vya kibaguzi kweli lakini haiwezi kufanya mabadiliko ya kimila katika tamko la
kisheria.
Ameeleza
kuwa WLAC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya jitihada zote za
kukata Rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini mnamo 2010 rufaa hiyo ilitupiliwa mbali
tena kwa kigezo kwamba uamuzi na amri iliyotolewa na mahakama kuu ilikuwa na
tarehe mbili Tofauti yani tarehe 8/9/2006 na tarehe 7/12/2006.
Amesema
kuwa baada ya jitihada zote hizo kugonga mwamba juu ya sheria hiyo kandamizi
ameeleza kuwa serikali ya Tanzania kuzingatia ukubwa wa swala hilo kufanya
marekebisho ya haraka kwani ndio chanzo kikubwa cha wanawake wajane nchini
Tanzania kushindwa kupata haki zao za msingi zikiwemo za mirathi baada ya vifo
vya wenzi wao
Mkutano huo ukiendelea |
Bi
Theodosia ameendelea kusema kuwa pamoja na jitihada nyingi mbalimbali
zinazofanywa na WLAC na wadau mbalimbali watetezi wa haki za wanawake bado
serikali haijaonyesha jitihada za maksudi za kutekeleza Taarifa /maamuzi ya
kamati ya mkataba wa CEDAW kuhusu sheria ya miradhi ya kimila na hali ya wajane
Tanzania ili kuhakikisha kwamba wajane wanapata haki zao.
Aidha
WLAC wameitaka serikali ya Tanzania kuwajengea uwezo majaji na waendesha
mastaka na watumishi wa mahakama na wanasheria kuhusu mkataba wa CEDAW na
umuhimu kwa kuzingatia haki za binadamu katika maamuzi yao.
Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini-PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI WA HABARI24 BLOG |
Pamoja
na hayo WLAC wameitaka serikali kuchapisha taarifa hiyo ya kamati ya CEDAW na
kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila potofu dhidi ya wanawake na
kuwatendea haki badala ya kuwanyanyasa kwa namna mbalimbali.
Hata
hivyo WLAC wameitaka serikali kutoa fidia ya kutosha kwa wajane waliohusika
katika kesi mkakati kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki zap.
No comments:
Post a Comment