Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na ujumbe wake wanaoendelea na ziara yao kikazi nchini Marekani wamekutana na uongozi wa juu wa taasisi mbili kubwa zinazofungamana na vyama viwili vikubwa vya siasa nchini hapa - International Republican Institute (IRI) chini ya Rais wake, Ambassador Mark Green, na National Democratic Institute for International Affairs (NDI) chini ya Rais wake, Kenneth Wollack, na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu hali ya kisiasa na mwenendo wa demokrasia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Mazungumzo na NDI pia yalimhusisha aliyekuwa Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika (former US Assistant Secretary of State for Africa) Johnnie Carson ambaye anaheshimika sana na ana ushawishi mkubwa katika duru za siasa na diplomasia za Marekani.
No comments:
Post a Comment