Friday, July 29, 2016

CHADEMA NYANDA ZA JUU KUSINI NA NYASA WASEMA WAPO TAYARI KWA OPARESHENI UKUTA


      Bw  Frank  Mwaisumbe
CHAMA   cha  Demokrasia  na maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) wameunga  mkono maazimio yote yaliyotolewa na kamati  kuu  cha Chadema  chini ya mwenyekiti wake   Taifa   Bw  Freeman  Mbowe  ya  kuazisha  oparesheni UKUTA .
 
Taarifa   iliyotolewa kwa  vyombo  vya habari  leo   na mwenyekiti wa  kanda   ya nyanda
za  juu  kusini Bw  Frank  Mwaisumbe alisema  wamepokea  kwa mikono  miwili maamizimio  hayo  ya  kuanzisha  oparesheni UKUTA  nchini  nzima  na  kuwa wapo  tayari  kwa  kushiriki .
 
“Kwa ujumla wake (Mkoa wa Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe) inaunga mkono maazimio ya Kamati kuu ya Chama Chetu iliyoketi tarehe 27/07/2016 ya kupinga vikali aina zote za udikteta zinazoendelea na kufanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)….. na kuwa tupo tayari kuona Demokrasia
ya  vyama vingi  nchini Tanzania inaendelea  kuimarika kama iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius kamabarage Nyerere, ambayo aliiacha ikiwa na amani na utulivu na kuwa nchi yenye kuruhusu mfumo wa vyama vingi”
 
Alisema  kuwa  kwa  kuwa Tanzania  ni  moja kati ya  nchi zinazoendeshwa  kwa mfumo  wa  vyama  vingi  ni  vema  chama tawala CCM  kuacha  kufinyanga  Demokrasia hiyo na  kuviacha  vyama  vyote  kufanya  kazi ya   kujiimarisha  kwa  uhuru na amani  badala ya  kuzuia  vyama  kuendesha mambo  yao .
 
Kwani   alisema ili  chama  kiwe  imara  na  chenye  nguvu  ya kuleta  ushindani ni   lazima  kuwekeza  kwa  wananchi  na hivyo kuanzishwa  kwa oparesheni UKUTA kutasaidia  Chama  chao kuwekeza kwa  wananchi kazi  ambayo  hata   CCM wamekuwa wakiendelea  kuifanya hadi  sasa .
 
Mwaisumbe  alisemutakuwa ni  uonevu  mkubwa  iwapo  serikali ya  CCM itazuia  Chadema  kuendelea  na  Oparesheni  UKUTA  wakati juzi Dodoma katika  Uwanja  wa  Jamhuri aliyekuwa mwenyekiti  wa CCM Taifa  Rais  Mstaafu  Dr  Jakaya  Kikwete alifanya mkutano  mkubwa ambao  kimsingi si mkutano wa kiserikali ila  ulikuwa ni mkutano wa Chama.
 
Alisema  siasa  safi  ni pamoja na kuruhusu vyama vyote kuendelea ujenga  vyama vyao ikiwa ni pamoja na kutawaliwa na uhuru wa kuongea na uhuru wa kukosoa bila kuvunja katiba ya nchi.
 
Bw  Mwaisumbe  alisema  wao kama Chadema kanda ya Nyasa watahakikisha   wanafanya  zoezi hilo la Oparesheni  UKUTA pasipo kuvuruga  amani  ya  nchi na  kuona mikutano  yao  yote inafanyika kwa uhuru na amani na  wapo  tayari  kuendelea  kulinda amani na utulivu.
 
“ sisi CHADEMA kanda ya Nyasa kwa pamoja tunajiunga na UKUTA Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania.. wa UKAWA na tupo tayari wakati wote kupambana na mtu yeyote anayevunja katiba na kuweka udikteta…. hii ni nchi yetu sote na tupewe uhuru kwa usawa bila kuvunja katiba ya nchi”

No comments: