Tuesday, July 5, 2016

KAMPUNI YA EMOTEC YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA ZA TEHAMA

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella, akielezea moja kati ya gunduzi za kampuni yake kwa wageni (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka minne ya Chinese Alumni Association.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella (kulia) akielezea moja kati ya gunduzi ya kampuni yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Profesa Elisante Ole Gabriel (Wapili Kulia) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka mine ya Chinese Alumni Association nchini hivi .
Kampuni mpya ya masuala ya TEHAMA nchini Tanzania, Emotec Limited yaeleza kuwa imejizatiti katika kutoa huduma bora na zenye ubunifu wa hali ya juu kwa wateja wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec, Bw. Mosses Hella imesema kuwa kampuni yake ina mpango wa kuwa inayoongoza katika utoaji wa huduma na bidhaa bora katika soko la TEHAMA nchini.

“Tumedhamiria kutoa bidhaa za gharama nafuu, huduma bora, za kibunifu na suluhisho kwa wateja wetu. Lengo letu kuu ni kuwa kampuni yenye ubunifu zaidi iliyojizatiti katika utoaji wa huduma bora na za gharama nafuu katika mausuala ya TEHAMA nchini.” Alisema Bw. Hella
Bw. Hella amesisitiza kuwa kampuni yake pia inayo dhamira ya kubuni, kutengeneza, kusambaza na kufanyia marekebisho vifaa mbalimbali vya umeme hususani simu za mkononi, tablet, kompyuta, router na modemu za intaneti pamoja na luninga ambapo wamejikita zaidi katika ubora.

Mbali na hayo aliongezea kuwa Emotec ni kampuni ya masuala ya TEHAMA inayotazamia pia kutoa huduma za vitabu kwa njia ya mtandao (e-content) katika kusaidia kuimarisha mfumo wa elimu nchini.

“Pia tunawekeza katika kubuni na kuchapisha vitabu kwa njia ya mtandao (e-content) kwa ngazi za elimu ya shule ya msingi, sekondari na ya juu ili kusaidia kuimarisha mfumo wa elimu nchini.” Alibainisha
Aliongezea pia shughuli nyingine ambazo kampuni yake inajihusisha nazo ni pamoja na kubuni, kufunga na kusaidia Maabara ya Usimamizi wa Mifumo wa Taarifa, Mifumo ya Usimamizi wa Mapato, Mifumo ya Usimamizi wa Taarifa za Shule, Mifumo ya Usimamizi ya Hoteli na mifumo ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao.

Kwa kuongezea zaidi kampuni pia imewekeza katika kubuni, kufunga na kusaidia mifumo midogo ya fedha na program tanzu ya kibenki lakini pia ina mfumo mzuri wa kimtandao kwa bandari, viwanja vya ndege na vituo vya makontena.

“Hivyo basi ningependa kuchukua fursa hii kuwaalika watanzania kutembelea banda letu katika maonyesho ya 40 ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo tunaonyesha bidhaa zentu zenye ubinifu na tekinolojia ya kisasa kabisa kwani hapo ndipo mahali wanapoweza kujua mengi zaidi kuhusu kampuni yetu.” Alihitimisha Bw. Hella

No comments: