Maelfu ya wananchi wakiwemo viongozi wa serikali na wa siasa wamejitokeza kumzika aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilindi mkoani tanga marehemu Beatrice Shelukindo yaliyofanyika nyumbani kwao kata ya Olorieni jijini Arusha.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na waziri wa afya Mh Ummy Mwalimu,waziri mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa,wabunge na pia viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini.
Wengine ni pamoja na Rais wa mahakama ya afrika Jaji Agustino Ramadhani,msemaji wa Chama cha Mapinduzi mh Christopher olle sendeka na wakuu wa mikoa na wilaya mbalimbali ambao wamemwelezea marehemu beatrice Shekukindo kama kingozi wa mfano.
Marehemu Beatrice Shelukindo ambaye ameacha mume na watoto watatu alikuwa mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya Ubunge wa Jimbo Kilindi 2005-2015 na Ubunge wa Bunge la afrika Mashariki 2001-2004.
No comments:
Post a Comment