Na
VICENT MACHA Dar es salaam
Chama
cha TANZANIA WOMEN CHEMBER OF COMMERCE(TWCC)kimetunikuwa tuzo ya taasisi bora inazowezesha ukuwaji wa
biashara katika kinya n’ganyiro cha saba katika vinyanganyiro Zaidi ya 18
vilivyokuwa vikigombaniwa katika maonyesho ya saba saba yaliyozinduliwa leo na
Rais wa Rwanda Mh PAUL KAGAME.
Akizungumza
na mwandishi wa mtandao huu katika maonyesho hayo Bi. Jacqueline Mneney Maleko
ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho amesema tuzo hiyo ni chachu kwa TWCC kuweza
kuongeza juhudi katika kutimiza wajibu wao na ni kwa mwaka wa kwanza tangu
achaguliwe kuwa mwenyekiti na kuwezesha kupata tuzo hiyo.
Mwenyekiti
huyo ameongeza kuwa kutokana na vigezo
walivyokuwa wakitumia kupata washindi hao ni pamoja na kuangalia ubora wa bidhaa na kuwahoji maswali wauzaji au watengenezaji wa
bidhaa hizo na pia hawakuwa na wasi wasi na kinyan’ganyiro hicho kwa kuwa
walijiandaa vya kutosha na walihakikisha wanaweza kushinda kutokana na
maandalizo hayo makubwa.
Aidha
mwenyekiti huyo amempongeza Bi KONSOLATA ambaye ni mwanamke pekee ambaye
aliweza kuchimba madini na pia kuyachonga jambo ambalo limekuwa nadra sana kwa
wanawake wa kitanzania kufanya na imezoeleka kufanywa na wanaume pekee lakini
kwa Mwanamke huyo ni Tofauti sana.
KONSOLATA alikuwa ni miongoni mwa watu
walioweza kuhojiwa na Mtandao huu ambapo amesema kuwa kitu kilichoweza kuwapa
ushindi ni umoja walio nao wana TWCC wote na pia TWCC iliweza kuwafundisha
kukabiliana na masoko ya kimataifa hivyo ni mbinu hizo zimewafanya kuweza
kuibuka washindi.
Maonyesho
ya saba saba yamezinduliwa leo na Rais wa Rwanda Mh PAUL KAGAME na Mwenyeji
wake Mh Rais MAGUFULI ambapo yakamalizika siku ya Tarehe saba ambapo ni kilele
cha siku ya Sabasaba Huku TWCC wakiwa ni moja kati ya wafanya biashara
wanaoshirika katika maonyesho hayo.
No comments:
Post a Comment