Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa maagizo mazito kwa watendaji wa Wizara hiyo kesho tarehe 22 Agosti.2016 kuhakikisha wanamfikishia taarifa ya kina kuhusu upungufu wa chanjo nchini.
Akiwa ziara ya kikazi Mkoani Geita, Ameagiza akute maelezo ya kina mezani kwake, kuwa ni nani haswa amesababisha chanjo kupungua kwenye maeneo mengi nchini? Na mpaka sasa amechukuwa hatua gani za kuwajibika?
Je, changamoto ipo hazina ama kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma za kinga? “Vyovyote vile, nataka utetezi uje ukiwa na vielelezo, kabla sijachukua hatua stahiki. Chanjo ni eneo pekee kwenye sekta ya Afya tulilofanikiwa kwa zaidi ya 95%! Haikubaliki kurudisha nyuma mafanikio haya."
Alisema, Baadhi ya maeneo chanjo zipo na wana dozi za mwisho na baadhi hazipo kabisa.
Mfano bohari ya chanjo Mkoa wa Geita hakuna chanjo za OPV, Rotavirus, BCG na Tetanus. Wangepaswa kuwa na akiba ya miezi mitatu mbele.
Kwenye ngazi ya Taifa wanapaswa kuwa Na chanjo za miezi Sita mbele, hapo ndipo tunaweza kusema tuna chanjo za kutosha.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Dk. Brayan Mawalla na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dk. Joseph Kisala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua sehemu ya dawa kwenye duka la Hospitali hiyo ya Mkoa wa Geita
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dk. Joseph Kisala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla katika ziara hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (hayupo pichani)
Mbunge wa Geita Mjini Mh. Constantine John Kinyasu akitoa maelezo kwa watendaji wa hospitali ya Mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo kwenye bohari ya dawa za chanjo ya mkoa wa Geita
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa maagizo kwa watendaji wa Wizara yake kuhakikisha wanampelekea maelezo ya kina juu ya upungufu wa chanjo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment