Tuesday, August 16, 2016

KINACHOENDELEA MAKAO MAKUU YA YANGA MUDA HUU--- TIZAMAHAPA

Baada ya Jana na leo habari za kujiondoa kwa mwenyekiti wa Club Ya yanga YUSUPH MANJI zikiendelea kuenea kwa kasi huku zikiwa zinadhibitishwa na wana yanga wa ndani ya Timu hiyo hatimaye leo wanachama wa Club hiyo mamia wameamua kujitokeza makao makuu ya timu hiyo kushinikiza mwenyekiti huyo asijiuzulu nafasi hiyo huku wakimtaka mzee maarufu wa Timu Hiyo Mzee Yahya Akilimali kufutwa uanachama mara moja.

Mtandao huu umepita maeneo ya jangwani na kushughudia mamia ya wanachama wengine wakiwa na mabango ya kumtaka mwenyekiti huyo kuendelea kuiongoza timu hiyo yenye maskani yake Jangwani Kariakoo Dar es salaam.

Aidha Habari zaidi zinasema katika vikao vya siri  vya viongozi wa Timu hiyo Vinavyoendenea ndani ya timu hiyo Maamuzi ya kumvua uanachama AKILIMALI yamnakaribia kufanyika huku wanachama wengi wakiwa wanashinikiza ifanyike Hivyo.

Mzee Akilimali Ndiye aliyetoa kauli Tata mbele ya wanahabari akiwabeza juu ya uamuzi wa Timu hiyo wa kumkodisha Manji Timu kwa miaka kumi ambapo aliwabeza kwa kusema kuwa Wamekurupupa kufanya hivyo.

Taarifa za kujiondoa kwa Manji zilianza kuenea jana Ambapo mwenyewe alinukuliwa na mitandao akisema kuwa amechoshwa na hataki tena lakini mpaka sasa hakuna Taarifa Rasmi inayoonyesha kukubali au kukataa kuendelea kuiongoza yanga.

TAARIFA ZAIDI ZITAENDELEA KUKUJIA UNGANA NASI KATIKA MITANDAO YETU YOTE YA Facebook,Insatagram na Twitter.Tumia jina Msaka habari




 


No comments: