TBC inakuletea kipindi kipya maalum ambacho kitawakutanisha wadau mbalimbali wakijadiliana na kuongelea umuhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma, kama ilivyoagizwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli.
Kutana na Marin Hassan Marin katika kipindi hiki, kitakachoanza Jumatano, tarehe 10 August 2016 na kuendelea kila siku ya jumatano saa 3:00 usiku TBC1, akikukutanisha watu mbalimbali katika kuchambua uamuzi huu muhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma.
Kutakuwa na maswali mbalimbali ambayo watazamaji watashiriki kuyajibu, na mshindi atajipatia zawadi kem kem.
Usikose kipindi hiki maalum, "SAFARI YA DODOMA" kila Jumatano saa 3:00 usiku TBC1
No comments:
Post a Comment