Tuesday, August 9, 2016

EXCLUSIVE VIDEO--GELINE FUKO AELEZA NAFASI ADIMU ALIZOZIPATA AKIWA KWA OBAMA MAREKANI




Baada ya GELINE kurejea Tanzania tulizungumza naye na kutueleza mambo kadhaa ambayo alifanyiwa akiwa Nchini Marekani .Video nimekuandalia hapo karibu
Geline Fuko amepata kutambulika baada ya Rais Obama kumtaja kama mfano wa kuigwa wa wanaharakati wa haki za binadamu wakati akizungumza Jumatano Agosti 3, 2016 katika kilele cha mpango wake wa kuwawezesha vijana wakiafrika unaojulikana kama Mandela Washington Fellowship. 

Raisi Obama alimsifu mwanasheria huyo kutoka LHRC ambaye ni moja  ya vijana 1000 waliokuwa jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo ili kuweza kusaidia Maendeleo katika Nyanja zote za maisha katika nchi zao.

RaisiObama alisifu juhudi za Gelineza kuibu awazo la kuanzisha kwa mara ya kwanza Kanzi data ya Katiba nchini Tanzania kwa kutekeleza wazo hilo chiniya LHRC. 

Raisi Obama alikaririwa akisema Marekani itaendelea kushikamana na wanaharakati kama Geline Fuko kutoka Tanzania. 

Geline ni mwanasheria namwanaharakati wa haki za binadamu ambaye amefanikisha kuanzishwa kwa Kanzi data ya Katiba ya kwanza na yapekee nchini Tanzania inayowawezesha watanzania kusoma Katiba kupitia simu zao za mkononi”.

Programu ya Mandela Washington Fellowship yenye lengo la kuwa wezesha vijana wa Kiafrika katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kijamii ilianzishwa na Rais Obama mwaka 2014. 

Programu hii hujumuisha vijana elfu moja (1000) kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao hugharamiwa na serikali ya Marekani kwenda jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo zaidi.


No comments: