Saturday, August 13, 2016

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam.

Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe. Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo leo Agosti 13, 2016 .

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto) akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.


No comments: