Mhariri wa EATV, Rwehabura Rugambwa akichangia hoja katika mkutano huo.
|
Mhariri kutoka kituo cha Mlimani TV Amini Mgheni (katikati) akichangia mada katika mkutano huo . Kushoto kwake ni Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Bi. Betty Kangonga |
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari. |
Wahariri wakichangia mada katika mkutano huo. |
Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP umekiri kuwa jitihada za uraghabishi zinazofanywa na Mtandao huo zimefanikisha kuwasaidia wananchi kujitambua na wengine kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuatilia miradi mbalimbali inayoelekezwa katika mitaa vijiji vyao.
Akizungumza na Wahariri mbalimbali katika mkutano maalum wenye lengo la kuboresha uelewa juu ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia, Mkurugenzi wa Mtandao huo Bi. Lilian Liundi alisema katika kata ambazo walifanikiwa kufika na kuwachokoza (kufanya ulaghabishi) kuhusu rasilimali zao na jinsi wanavyoweza kufanya mabadiliko ya kimaendeleo, asilimia kubwa waliweza kubadilika na kujiletea maendeleo.
Alisema mchakato wa ulaghabishi umeleta mabadiliko katika jamii ikiwamo kubadilisha hali yao ya kimaendeleo hususani katika sekta ya shule, maji na afya, kwani kuna baadhi za kata zilifanikiwa kubadilisha hali za shule zao kwa kupitia nguvu zao wenyewe na serikali kumalizia sehemu iliyobaki
No comments:
Post a Comment