Wanafunzi wa shule za msingi mbalimbali mkoani Dar es salaam wakishangilia kwa furaha wakati wa ziara ya wanafunzi hao waliyoifanya katika mamlaka ya reli Tanzania na Zambia TAZARA ambapo ziara hiyo ni moja ya shamra shamra za kuadhimisha miaka 40 tangu kuanza kwa mamlaka hiyo.Akizungumza na ,mtandao huu afisha Uhusiano wa Tazara kwa Upande wa Tanzania Bi Regina Tarimo amesema kuwa wanafunzi zaidi ya mia Tano wamepata nafasi ya kutembelea Mmlaka hiyo na kujionea utendaji kazi wa Reli za Tazara ambapo pia walipata nafasi ya kupanda Treni moja wapo kutoka Makao makuu ya Tazara hadi Kituo cha MWAKANGA na kurejea ikiwa ni moja ya Tukio la kuwafanya wanafunzi kuelewa kwa undani Jinsi TAZARA inafanya kazi zake hapa nchini |
|
No comments:
Post a Comment