Mambo kadhaa yaliyojadiliwa ndani ya baraza la madiwani Temeke leo
Baraza
la Madiwani ni moja ya chombo muhimu cha kutetea maslahi ya wananchi
kupitia uwakilishi wa madiwani wao, na mabaraza mengi nchini yamekuwa
yakichukua hatua mbalimbali pale wanapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo
kwa maslahi yasiyokuwa ya wananchi.
Ambapo
siku ya leo katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya
Temeke chini ya Mstahiki Meya Abdalah Chaurembo, limezungumza masuala
mengi yenye tija kwa Taifa ikiwemo suala la muwekezaji wa kiwanja cha
Osterbay maarufu kama 3 Star ambaye aliingia mkataba tangu mwaka 2013 na
kwa mujibu wa mkataba huo ilibidi eneo hilo liendelezwe kwa kuwa
kitega uchumi ambacho kitaliingizia pato Halmashauri lakini imekuwa
ndivyo sivyo.
Akichangia
suala hilo Naibu Mstahiki Meya Salum Feisal Hassan, ameeleza kuwa
muwekezaji huyo amevunja mkataba hivyo hatua stahiki inabidi zichukuliwe
kwani amekuwa kama dalali wa kutafuta wawekezaji wengine waliendeleze
eneo hilo, badala ya yeye mwenyewe kuwa na uwezo binafsi wa kufanya
hivyo kama mkataba unavyoeleza.
Katika
hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Temeke ambaye anaingia kama mjumbe
kwenye Baraza la Madiwani Abdallah Mtolea, amewataka madiwani kujifunza
sheria na kanuni za mabaraza ya madiwani, ili kuleta maelewano yenye
tija kwa Halmashauri hiyo, jambo ambalo Mstahiki Meya Chaurembo ameeleza
kuwa limetengewa bajeti na zoezi la semina litaanza hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment