Thursday, August 25, 2016

MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YAAGWA LEO KUPELEKWA MIKOANI KWA MAZISHI.

Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa  kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi .Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  Polisi  vilivyopo  barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa  askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.

Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba  miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi    katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi  vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, akizungumza wakati wa maombolezo na kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi.Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.

No comments: