Kituo cha sheria na
haki za binadamu nchini Tanzania LHRC kimelaani vikali maneno yanayotolewa na
baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali maneno ambayo wamedai yanazidi kuchochea chuki na
uhasama miongoni mwa watanzania na kujenga hofu kubwa katika nchi.
Hayo yemeelezwa ikiwa
nchini Tanzania kuna vugu vugu kubwa la kisiasa huku kambi mbili za kisiasa
ambazo ni chama kikuu cha upinzani na serikali wakijibishana kwa kauli
mbalimbali kuhusu maandamano ambayo yamepangwa kufanyika na chama kikuu cha Upinzani
CHADEMA wiki ijayo.
Akizungumza na
wanahabari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Hellen Kijo
Bisimba amesema kuwa kumekuwa na kauli kali na za kutisha zinazotolewa na
baadhi ya wanasiasa na Viongozi wa serikali ambazo zisipozuiliwa zinaweza
kulifarakanisha taifa na kujenga chuki kubwa.
Amesema kuwa
kumwekuwepo na hali ya kutishiana baina ya viongozi wa vyama,viongozi wa
serikali,,jeshi la polisi na raia kwa kauli hizo zenye kuleta hofu kwa raia
wanachama na wasio wanachama wa vyama vya siasa hasa kutokana na watanzania
kutokuwa na uzoefu wa lugha hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC IMELD LULU URIO(kulia) akisisitiza Jambo wakati wa mkutao huo wa wanahabari |
Akitolea mfano wa Lugha
ambazo zimekuwa zikitolewa siku za hivi karibuni ni pamoja na maneno kama
Udicteta Uchwara,UKUTA, Kuwashughulikia, Viberiti vya Gesi, Sijaribiwi, Tumejiandaa
kufa,Kuvunjwa Miguu,Kuwekwa ndani na maneno mengine ambayo wanadai hayastahili
kutumika katika nchi ambayo inatajwa kuwa kisiwa cha amani Africa.
Aidha Mama Hellen
ameongeza kuwa siku za hivi karibuni tumeshudia jeshi la polisi nchini ambalo
jukumu lake ni la kikatiba na kisheria ni kulinda Raia na mali zao likijipambanua
kama jeshi la kupambana na wananchi na kufanya mazoezi na majaribio ya vifaa
vya jeshi hilo kwenye mitaa na makazi ya watu wakilipua milipuko bila sababu za
msingi hali ambayo imewajaza hofu wananchi ambao hawaelewi kinachoendelea.
“Mfano akiwa Ziarani
mkoani singida alituoa Tamko la kuzuia mikutano na shughuli za kisiasa hadi
mwaka 2020 jambo ambalo ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa na katiba ya
nchi”amesema Hellen.
LHRC wamelitaka jeshi
la polisi nchini kuzidi kuimarisha dhana ya polisi Jamii iliyoasisiwa miaka
michache Iliyopita ili kusaidia katika kuimarisha ulinzi wa Raia na mali zao.
No comments:
Post a Comment