Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo Spika mstaafu Mama Anna Makinda akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa wanawake |
Wakati wanaharakati wa
haki za wanawake na wadau mbalimbali wakiendelea kupambana kuhakikisha kuwa
wanawake wanapata nafasi sawa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ya
uongozi,rushwa ya ngono,Umaskini vimetajwa kuwa vikwazo vikubwa vinavyofanya
taifa la Tanzania kushindwa kuwa na wanawake wengi katika nafasi mbalimbali za
kisiasa.
Hayo yameelezwa Jijini
Dar es salaam na wakawake viongozi na wanaotarajiwa kuwa viongozi katika
kongamano maalum la wanawake lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP
kwa kushirikiana na ACTIONAID mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake
hao kupambana katika nafasi mbali mbali za uongozi nchini.
Katika Tamko
lililosomwa na wakawake hao mbele ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Spika mstaafu
ya Bunge la Tanzania Mama ANNA MAKINDA wanawake hao wameeleza kuwa uwezo mdogo wa
kiuchumi miongoni mwa wanawake walio wengi umekuwa kikwazo kikubwa sana katika
harakati zao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za nchi na
kujikuta wakishindwa kushiriki kwa ukamilifu zoezi la uchaguzi jambo ambalo
linazidi kuwapa nafasi wanaume kutawala katika nafasi mbalimbali za uongozi
nchini.
Aidha wameeleza kuwa
kwa uzoezi walioupitia katika uchaguzi kwa mwaka jana imeeonyesha kuwa Rushwa ya ngono ilikuwepo kwa kiasi cha
kuwakwamisha baadhi ya wanawake na wengine kuogopa kujitokeza katika nafasi
hizo huku pia familia zikishindwa kuwaunga mkono wanawake wanaotaka kugombea
kwa kile walichoita ni kuogopa aibu ya rushwa ya ngono kwa familia.
Wanawake mbalimbali wakichangia mijadala katika shughuli hiyo |
Wanawake hao ambao walikutana
kwa mara ya kwanza Mjini Dodoma mwaka 2015 kabla ya uchaguzi mkuu na baaadae
kukutana Wiki hii kupeana mrejesho wa kile kilichotokea katika uchaguzi mkuu wa
mwaka jana wamesema kuwa wanaitaka serikali Asasi za kiraia,TAKUKURU na wadau
wengine kuongeza jitihada za kukemea Rushwa ya ngono na kuongeza uhamasishaji
ili iweze kuzunguziwa kwa uwazi ili kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria
katika kulishughulikia Tatizo hilo.
Aidha wanawake hao
wameitaka serikali kurekebisha sheria ya usajili wa vyama vya siasa ya mwaka
1992 itamke rasmi uwiano na usawa wa kijinsia katika nafasi kuu za maamuzi
ndani ya vyama na pia sheria ivitake vyama vya siasa kuteua wanawake asilimia
50 kwenye kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi Taifa.
Katika warsha hiyo
ambayo mgeni Rasmi alikuwa Mama Anna Makinda wengine waliohudhuria ni pamoja na
Mgombea Pekee wa nafasi ya Urais mwanamke kutoka Tanzania Mama Anna Mgwira
Kutoka ACT WAZALENDO,mbunge wa viti maalum kutoka CHADEMA Sophia Mwakagenda,pamoja
na mkurugenzi mtendaji wa TGNP Bi LILIAN LIUNDI.
No comments:
Post a Comment