Ikiwa ni siku moja tu kupita
Tangu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda Kuwaagiza askari wa FFU na
viongozi wa ulinzi ndani ya Dar es salaam kuhakikisha wanazima haraka mipango
yote inayofanywa na chama cha CHADEMA ya kutaka kufanya mikutano katika
operationi yao waliyoipa jina la UKUTA,hatimaye Uongozi wa baraza la vijana
Chadema BAVICHA wameibuka na kupuuza agizo hilo huku wakisisitiza kuwa
maandalizi ya kuelekea September moja yamekamilika na watanzania wajiandae
kudai haki yao.
Akizngumza na
wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Bavicha Taifa PATROBAS
KATAMBI amesema kuwa kauli ya mkuu wa mkoa ni ya kupuuzwa kwani hana mamlaka
kisheria sio tu kuzuia mikutano bali hata kuruhusu bali mwenye mamlaka hiyo
kisheria ni OCD hivyo watanzania wasitishwe na wajitikeza kwa wingi.
Amesema kuwa wao kama
Vijana wa chadema walipokea agizo la viongozi wao wakuu wa chama la kufanya
maadalizi ya kufanya mikutano nchi nzima ifikapo September moja na wao wakaanza
maandalizi mara moja na tayari maandalizi hayo yamekamilika na wanajiandaa
kufanya mikutano hiyo.
Chama cha CHADEMA
kimepanga kufanya mikutano yake nchi nzima ifikapo September Moja kwa lengo la
kupinga mfumo unaotumika na Serikali ya awamu ya Tano wanaodai kuwa ni mfumo wa
Kidikteta na operation hiyo imepewa jina la UKUTA.Mpaka sasa mikutano hiyo
imeanza kupigwa marufuku na viongozi wa serikali akiwemo Rais magufuli na Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam lakini CHADEMA wanasisitiza kuwa watafanya mikitano
hiyo
No comments:
Post a Comment