Friday, August 19, 2016

SERIKALI YASEMA WANAOWAPA MIMBA WATOTO WA SHULE NA KUWAOA HATA MAGEREZA YAKIJAA WATAENDELEA KUKAMATWA

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya pili Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi kutoka Shirika la CDF, Kashuma Mtengeti, Mwakilishi wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane Miller na Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Mwakilishi wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane Miller, akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Wazir Ummy Mwalimu (kulia)
 Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu (kulia), akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa taarifa ya mradi huo.
 Wadau mbalimbali na waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Mwakilishi kutoka Shirika la MBE FORWARD UK-Naana Otoo Oyortey akitoa mada kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi huo.
 Mwakilishi kutoka Shirika la CDF, Kambibi Kamugisha, akitoa mada.
 Waziri Ummy Mwalimu akihutubia kabla ya kuzindua rasmi 
mradi huo

 Mwakilishi kutoka Wadada Centre, Christian Noah akitoa mada kwenye uzinduzi huo
 Mkurugenzi kutoka Shirika la CDF, Kashuma Mtengeti, akichangia jambo.
 Waandishi wa habari wakiwa kazini.
 DK. Flora Myamba kutoka Repoa akitoa mada kwenye 
uzinduzi huo.
Christine Mwanukuzi kutoka shirika la UNFPA, akichangia jambo.


Na Dotto Mwaibale


SERIKALI imesema hata magereza zikijaa itaendelea kuwakamata na kuwachukulia sheria kali wanaume wote wataka0 bainika kuwaoa au kuwapa  mimba wanafunzi.

Hayo yalisema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akizindua mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya pili Dar es Salaam leo.

Mwalimu alisema kuwa hata magereza yakijaa kwa kiasi gani serikali haitasita kuwakamata watuhumiwa hao bila ya kuwaonea huruma bila ya kujali mtuhumiwa ni mtu wa namna gani.

"Nawaagiza maofisa Ustawi wa Jamii wote katika ngazi ya mikoa, wilaya na Kata kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa nchini kote hususan mtoto wa kike. Ninataka wahakikishe wale wote wanao wapa watoto wa shule mimba na wanao waozesha au kuoza wanakamatwa na kuchukuliwa hatua haraka kwani sheria za kuwalinda watoto zipo, kinachotakiwa sasa ni utekelezaji" alisema Mwalimu.

Waziri Mwalimu alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha ndoa za utotoni ambapo taarifa ya Demografia na Afya ya mwaka 2010 zimeonesha kuwa kwa wastani wanawake 2 kati ya watano Tanzania wa umri wa miaka 15-49 waliolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Aliongeza kuwa utafiti wa hali ya afya ya uzazi, mtoto na malaria wa mwaka 2015/16 unaonesha kuwa idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19 imeongezeka kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010 na kuwa tatizo hilo lipo zaidi katika mikoa ya Katavi kwa asilimia 36.8, Tabora, asilimia 36.5, Simiyu asilimia 32.1, Geita asilimia 31.6 na Shinyanga kwa asilimia 31.2.

Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu alisema katika kudumisha harakati za kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni vinavyoendelea kuwakumba wasichana nchini Tanzania, CDF, Chama cha Uzazi na Malezi (Umati) na Kituo cha Wadada Centre wameamua kuzindua mradi huo kwa pamoja ili kulinda haki za wasichana hapa nchini.



No comments: