Serikali imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane nchini.
Akizungumza hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.
“Serikali kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia viwanda,” alisema Mhe. Ummy.
Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali zitokananzo na dawa hizo.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini (TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na ubora unaopaswa kutumiwa na Watanzania.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.
Mbali na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi zaidi ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga hatua kiuchumi ili isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri na watayafanyia kazi kwa haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA KAZI TU”.
“Tumepokea maagizo ya Mhe. Waziri na nataka kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha maendeleo na Afya bora” alisisitiza Dkt. Moses.
No comments:
Post a Comment