Mtandao wa mashirika
yanayopinga ndoa za utotoni ni mtandao unaoundwa na asasi zisizokuwa za
kiselikali zipatazo 32 hapa nchini. Mtandao huu umekuwa ukifanya kazi
mbalimbali katika ngazi ya kijamii mpaka ngazi ya kitaifa ili kuondokana na ukatili
wa watoto ikiwemo ndoa za utotoni.
Mwanzoni mwa mwaka huu
taasisi ya mwanamke initiative ambayo ni mwanachama wa mtandao huu ulifungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu ya
Tanzania, shauri namba 5 la mwaka huu 2016 ikiwa ni kati ya Rebeca Gymu (Mkurugenzi
mtendaji wa taasisi hiyo) na mwanasheria
mkuu wa serikali.katika kesi hii mlalamikaji alikuwa akihoji uhalali wa kikatiba wa vifungu namba 13 na 17
vya sheria ya ndoa ya mwaka 1997 iliyokuwa ikieleza kuwa mtoto wa kike
anaruhusiwa kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 au 15 kwa ridhaa ya wazazi au
mahakama.
Valeria Msoka
mwenyekiti wa Mtandao wa kupinga ndoa za utotoni Tanzania alisema wao wakiwa
kama watetezi wa haki za watoto na wanaopinga ndoa za utotoni walifurahishwa na
hukumu iliyotolewa mapema Julai 8,2016 chini ya jaji mkuu Shabani Lila ambapo alisema
vifungu hivyo sio halali kwa mujibu wa katiba na kuitaka serikali kubadilisha
ndani ya muda wa mwaka mmoja.
Alisema wao kama Taasisi
inayopinga ndoa za utotoni walishangazwa na walishtushwa na tamko la
mwanasheria mkuu wa selikali kuwa amekata rufani katika mahakama ya rufani ili
kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama kuu kwenye kesi hiyo.
Aidha aliendelea kusema
kuwa wao wameshindwa kuelewa rufaa hii inabebwa na misingi gani na je ni kweli
selikali ya Tanzania inataka kuendelea kuwa na vifungu hivi vinavyosema kuwa
mtoto wa kike aweze kuolewa chini ya
miaka 18.
April 27 waziri wa
katiba na sheria alizungumza bungeni kuhusu dhamira ya selikali kupeleka
mswaada bungeni kupinga ndoa za utotoni akijibu swali la mbunge wa ileje
aliyetaka kujua ni lini selikali itafanya marekebisho ya sheria ya ndoa nchini,
wao wakiwa kama wanamtandao na wanaopinga ndoa za utotoni walitegemea kwenye
hili selikali ingeamua kuchukua shauri la mahakama kuu na kuboresha sheria hiyo
lakini matokeo yake selikali yenyewe ndio inaenda kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Aliendelea kusema ikumbukwe kuwa Tanzania ni nchi
mwanachama wa umoja wa mataifa na umoja wa afrika na iliridha mikataba mbalimbali ya kikanda na ya kimataifa ya kulinda haki na
ustawi wa mtoto na kupinga aina zote za ukatili na ubaguzi dhidi ya
mwanamke.mikataba hiyo ni pamoja na mkataba wa haki za mtoto wa kimataifa wa mwaka 1989 pamoja na mkataba
wa afrika wa haki na ustawi wa mtoto pia wa mwaka 1990,hivyo kama selikali ina
haki ya kutunga sheria kama wajibu wa utekelezaji wa sheria hii kwani ndoa za
utotoni ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ni ukatili wa wanawake na watoto wa
kike.
Tafiti mabailmbali
zilizofanyika zinaonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya ndoa za utotoni kwa takribani 35% ndoa za utototoni ni janga
la kitaifa na zinamadhara makubwa kwa
mtoto mwenyewe hata jamii nzima.
Ndoa za utotoni husababisha
mimba za utotoni zenye kumuathiri mtoto wa kike kwa mfano tarehe 2 julai 2012
taasisi ya Tanzania life Improvement Association (TALIA) ilitoa taarifa kwamba
kulingana na takwimu za wizara ya elimu, mafunzo ya ufundi, kila mwaka
wasichana 8,000 huacha masomo kutokana na mimba za utotoni. Aidha kila mwaka 24% ya wanawake wajawazito
hufa kutokana na matatizo ya mimba za utotoni na aslilimia 5 mpaka 6 ni watoto
wa kike wenye umri chini ya miaka 18.
Inapozungumziwa nafasi
ya mwanamke hapa nchini Tanzania na changamoto anazokutana nazo kiuchumi
,kisiasa na kijamii msingi wake pia hutokanana na mambo kama haya ya ndoa chini
ya miaka 18. Mtoto wa kike ananyimwa fursa ya kukua na kufurahia utoto wake,
fursa ya kupata elimu , fursa ya kujitambua na hata ya kujiinua kiuchumi kwani
ndoa za utotoni huua kabisa ndoto za mtoto huyo.
Madhara mengine
yatokanayo na ndoa za utotoni ni ukatili wa kijinsia kwani watoto hawa uozeshwa
kwa watu waliowazidi sana umri. Ndoa za utotoni zina madhara kiafya ikiwemo
kupoteza maisha, kupata shida wakati wa uzazi, maambukizi ya magonjwa ikiwemo
ukimwi na hata malezi duni kwa watoto wanaozaliwa na mama huyo kwa kuwa na yeye
bado ni mtoto hivyo basi kwa kuzingatia yote haya tunashangazwa sana na
selikali inapinga maamuzi ya kubadilishwa kwa sheria kama vile walioko
selikalini hawatambui madhara haya au wanayafurahia
Wao kama wana mtandao wanapenda kuikumbusha
selikali kuwa ni jukumu lao na ni wajibu kulinda haki za Raia na makundi mbalimbali katika jamii. Ulinzi huu unaweza kufanyika pale tu
panapokuwa na misingi imara ya kisheria hata kiutawala na kimfumo ili
kuhakikisha sheria zinasimamiwa ipasavyo.
Anasema kuwa Ni aibu
kubwa sana taifa kuwa na sheria katika karne hii inayotamka wazi mtoto mwenye
umri chini ya miaka 18 anaweza kuolewa. pia selikali ikumbuke kuwa imeridhia utekelezaji
wa mipango endelevu ya maendeleo 2030 pamoja na ajenda ya umoja wa afrika 2063
vya kuondokana na vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto
,kiuchumi, na kisiasa.ili kuweza kutekeleza mipango na mikakati hii selikali inawajibu
wa kuhakikisha kuwa inaweka misingi thabiti ya sheria na usimamizi wa sheria
hizo. Wanamtandao wanaishauri selikali iondoe kusudio hilo la kukata rufaa na
ijipange kutekeleza amri ya Mahakam kuu.
No comments:
Post a Comment