Wakati watanzania
wakisubiri kwa hamu ahadi ya serikali ya awamu ya tano iliyoingia nayo
madarakani ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda mpango huo umeelezwa kuwa
unaweza kufeli kama serikali haitajikita katika kutengeneza wanasayansi vijana kuanzia
shule za msingi na secondary ili baadae waje kuwa tegemeo katika viwanda hivyo
nchini.
Hayo yameelezwa leo
Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa shirika la
wanawasansi chipukizi Tanzania YST Dr Gozibert Kamugisha wakati akizungumza na
wanahabari kuhusu onesho la wanasayansi chipukizi la mwaka 2016
litakalofanyika katika ukumbi wa Julias Nyerere Jijini Dar es salaam kuanzia
tarehe 10 hadi 11 mwezi huu wa nane tukio ambalo litawakutanisha wanafunzi
mbalimbali kuonyesha kazi za ugunduzi wa kisayansi na teknologia
zilizotengenezwa na wanafunzi wa shule za secondary kutoka mikoa yote Tanzania
Amesema kuwa mpango huo
wa kuwakutanisha wanasayansi kutoka mashuleni na kuwapa nafasi ya kuonyesha
kazi zao utakuwa msaada mkubwa kipindi
kijacho na hasa kipindi hiki ambacho serikali ya Tanzania inataka kuingia
katika mfumo wa kuwa nchi ya viwanda huku akisema kuwa kama serikali haitaweza
kuwakuza wanasayansi kutoka katika mashule na vijana mpango wa viwanda hauwezi
kufanikiwa kamwe kwani wanaoendesha viwanda kote duniani kwa asilimia kuwa ni
wanasayansi.
Co-Founder/Director and senior science Adverser kutoka shirika la wanasayansi chipukizi Tanzania YST akikisiriza jambo mbele ya wanahabari |
Katika maonyesho hayo
yatakayofanyika Dar es salaam wanafunzi ambao watafanya vizuri kwa kuonyesha
Bidhaa bora Zaidi wataibuka na zawadi mbalimbali ambapo wanafunzi wapatao 50
watashinda zawadi ya Pesa,Medali,vikombe,vifaa vya maabara na kutengeneza maktaba
kwa shule itakayoshinda zawadi ya maktaba.
Kamugisha ameongeza
kuwa wanafunzi wanne watashinda zawadi ya udhamini wa kushomeshwa chuo kikuu
katika fani ya sayansi ili kuwawezesha kuwa wanasayansi mahiri miaka ya baadae
huku akisema kuwa washindi wa Jumla wa mashindano ya mwaka huu watalipwa
Gharama zote za kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya BT YOUNG
SCIENTISTS huko ulaya nchini Ireland mwezi January 2017 na pia watapewa
Udhamini wa kusomeshwa chuo kikuu.
No comments:
Post a Comment