Thursday, September 1, 2016

SHULE NNE ZA WILAYANI GEITA ZAPIGWA “TAFU” YA MADAWATI NA TIGO FIESTA

 Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga (kushoto)akipokea moja kati ya madawati 185 yenye thamani ya shillingi milioni 31 jana, toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande ikiwa ni mpango wa kampuni ya simu za mkononi Tigo kutoa madawati kupitia kauli mbiu “ Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora fiesta 2016 kwa kishindo cha Tigo imooo”

Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga(katikati)  akiwa ameketi kwenye dawati mara baada ya kukabidhiwa madawati 185 toka kampuni ya simu za mkononi Tigo hafla iliyofanyika shule ya msingi Mwatulole jana mkoani humo, Wengine pichani kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande na Afisa elimu mkoa wa Geita, Catheline Mashala.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga akiwa ameketi na wanafunzi wa shule ya msingi Mwatulole mara baada ya kukabidhiwa madawati 185 toka kampuni ya simu za mkononi Tigo hafla iliyofanyika shule ya msingi Mwatulole jana mkoani humo, Pembeni mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi.

 Geita, Agosti 30, 2016:  Kampuni ya Tigo Tanzania  leo imekabidhi madawati 185 yenye thamani ya shilingi milioni 31  yatakayogawiwa shule nne katika mkoa wa Geita  ikiwa ni sehemu ya mkakati wake unaoendelea nchi nzima wa kutoa msaada wa madawati  ambayo yatainufaisha mikoa 14 bega kwa  bega na tamasha la Tigo FIESTA 2016.  
Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’
Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo  zilizofanyika katika Shule ya Msingi Mwatulole, Meneja wa Kikanda wa Tigo Kanda ya Ziwa Edgar Mapande, alisema  umekuwepo uhitaji mkubwa wa madawati katika shule za msingi na kutokana na kuwepo kwa uhaba wa madawati  imebainika kuwa ni moja ya sababu zinazoathiri uwezo wa kujifunza  pamoja na ufanisi wa masomo miongoni mwa  wanafunzi  katika  shule zetu nyingi za msingi.
“Lengo letu kama kampuni ni kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi na tunayo furaha  kwamba msimu wa FIESTA 2016 unaleta mabadiliko kwa  kizazi cha baadaye  ambacho ni wanafunzi walio katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai tena chini sakafuni,” alisema Mapande.
Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu  Ezekiel Kyingu     ambaye alisema kuwa madawati hayo 185 yataboresha kwa kiwango kikubwa  mazingira ya kujifunza  kwa watoto katika mkoa huo  na kutoa witom kwa watu wengine wenye mapenzi mema  kujitokeza  na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mashule  mkoani humo.
Kyingu  alizitaja shule  zitakazonufaika na  madawati hayo  na idadi yake katika mabano kuwa ni Mwatulole (50), Nyankumbu (45), Ukombozi (45),  na Kivukoni (45).
 “Tunawashukuru sana Tigo  kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza idadi ya uhaba wa madawati  katika shule za msingi mkoani Geita. Tunaamini  madawati haya 185  yatatufikisha mbali  katika  kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio katika kuelekea kuwa viongozi wa baadaye,” alisema Kyingu.

 Mradi mkakati wa madawati wa Tigo Fiesta ulianzia mkoani Mwanza na hadi sasa Tigo imeshatoa madawati wilayani Kahama na mkoani Kagera.

No comments: