Monday, October 10, 2016

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe7 Oktoba 2016.

Mary Kinabo -Afisa Mwandamizi wa Soko la Hisa DCE akizngumza na wanahabari Jijini Dar es salaam
Mauzo ya Soko
Mauzo yameongezeka kwa 65% kutoka TZS 19.6 Bilioni kufikia TZS 32.5 Billion.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimepanda mara 4 zaidi kutoka 2.4 millioni kufikia 9 millioni

Makampuni yanayoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
CRDB ………………………………………..70%
TCC …………………………………… 25%
TBL …………………………………………3%

Mtaji wa Soko la HISA
Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa 0.41% kutoka Trilioni 21.579 hadi Trilioni 21.49 umechangiwa na kushuka kwa bei kweny kaunta za NMG & ACA
Mtaji wa makampuni ya ndani umepanda  kwa 0.35% kutoka Trilioni 8.1 hadi Trilioni 8.13 umechangiwa na kushuka kwa bei kweny kaunta za TBL

Viashiria (Indexes)

Sekta ya viwanda (IA) wiki hii imepanda kwa pointi 26.16 baada ya bei za hisa za TBL kupanda kwa 0.77%.

Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imeshuka pointi 0.52 baada ya bei kushuka kwenye kaunta za DSE kwa 1.54%.


Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imeshuka pointi 4.19 baada ya bei kushuka kwenye kaunta za Swissport kwa 0.12%.


No comments: