Friday, October 28, 2016

MICHEZO YA LIGI KUU MWISHONI MWA WIKI

Wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiendelea leo Ijumaa Oktoba 28, 2016 kwa mchezo mmoja, kwa siku ya kesho Jumamosi Oktoba 29, mwaka huu kutakuwa na michezo mitano wakati kwa siku ya Jumapili kutakuwa na michezo miwili—michezo yote ikiwa ni ya raundi ya 13, ligi ikielekea ukiongoni mwa mzunguko wa kwanza.

Leo Kagera Sugar inacheza dhidi ya Azam FC katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati kesho itakuwa ni zamu ya Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City ya Mbeya itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mwadui ya Shinyanga inatarajiwa kuialika Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu na Ndanda zitachuana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Keshokutwa Jumapili Oktoba 30, 2016 Young Africans itacheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

No comments: