Saturday, October 29, 2016

RC -PAUL MAKONDA AONGOZA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARY JITEGEMEE JKT MGULANI JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora,  Samuel Ndebeto.
RC Makonda akipeana mkono na mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Samina Rajab baada ya kumkabidhi cheti  katika mahafali ya 32 kwa ushiriki wake wa masuala ya Skauti shuleni hapo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
Huyu ndiye ni Mwanafunzi Bora wa Shule hiyo,  Samuel Ndebeto.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali. Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali, Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.
Mgeni rasm Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhitimu wa kidato cha nne akisakata rhumba kwenye mahafali hayo.
Walimu na wanafunzi wakicheza kwaito.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu ndani ya ukumbi.
Mgeni rasmi Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa jukwaa kuu.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya shule hiyo.


Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi na walezi kuwaacha huru watoto wao kuendelea na masomo wayapendayo badala ya kuwachagulia.

Mwito huo ameutoa katika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Jitegemee JKT Mgulani Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Watoto wapewe uhuru wa kile wanachopenda kukisomea badala ya kuwachagulia kwa kufanya hivyo itawasaidia kupenda kazi watakayoifanya kutokana na masomo waliyosoma" alisema Makonda.

Alisema hivi sasa kuna changamoto kubwa kwa watumishi kujiingiza katika vitendo vya ubadhirifu kutokana na kutokuwa wazalendo kutokana na kufanya kazi ambayo imetokana na masomo ambayo hawakuyapenda.

Alisema kama mtoto anapenda kuwa mtaalamu wa kompyuta muache aendelee na masomo ya kompyuta badala ya kumlazimisha kuwa na taaluma nyingine.

Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy alisema wahitimu hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mtihani wao watakao uanza Jumanne wiki ijayo na kuwa wanategemea wote watafanya vizuri.

Kessy alisema kuhitimu kidato cha nne ni hatua nyingine ya kuendelea na elimu ya juu hivyo aliwataka wahitimu hao kuondoa wasiwasi katika kipindi hiki cha kuelekea kufanya mtihani wa mwisho.

Wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi Paul Makonda wanafunzi hao walisema changaoto kubwa waliyonayo na uchakavu wa miundombinu shuleni hapo kama mapaa ya vyumba vya madarasa kuezekwa kwa mabati aina ya Asbestors ambayo si mazuri kiafya pamoja na uchakavu wa sakafu ambapo Makonda aliahidi kutoa mabati 2,000 kwa ajili ya kuezekea vyumba 25.

Katika hatua nyingine Makonda amezitaka shule za sekondari za jeshi katika mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha zinaunda kamati kwa ajili ya kurudisha heshima ya michezo mashuleni kama ilivyokuwa awali.

No comments: