Thursday, October 20, 2016

TFF YATOA UFAFANUZI SAKATA LA HASSANI KESSY,YANGA HAIWEZI KUKATWA POINTI.

Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Hatimaye Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu nchini Tanzania [TFF] limeamua kulitolea ufafanuzi sakata la beki Hassani Ramadhan Kessy kuhusiana na Madai ya timu ya Simba ya mchezaji huyo kuvunja mkataba na kujiunga na Yanga.

Akiongea na waandishi wa habari wa TFF Alfred Lucas,amesema kuwa mchezaji huyo yupo huru kuitumikia Yanga katika michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania bara hata kamati ya hadhi ya wachezaji ilimuidhinisha kuichezea klabu yake kwa sababu uongozi wa Simba haukuwasilisha kesi ya kuhusiana na maswala ya usajili ila ilileta swala la kuvunja mkataba.

“Kessy ni mchezaji halali wa Yanga ila tu kuna malalamiko ya pande mbili ya kwanza ni Simba kudai kuwa alivunja mkataba kwa makusudi na pili Kessy anailalamikia Simba hivyo kamati imeamua kutafuta suluhisho kati ya wawkilishi wa vilabu hivyo kukaa kwa pamoja na kutatua sakata hilo na kama watashindwa kuelewana basi TFF tutatumia kanuni na sheria zinasemaje”alisema Lucas.

Aidha Lucas amesema kuwa anashangaa kuona kwenye mitandao ikipotosha umma kuwa Yanga watakatwa pointi kwa kumchezesha Kessy ni uzushi kwani mchezaji huyo hana kosa kuhusiana na maswala ya usajili ila tu Simba ina madai kwa kuvunja mktaba na inataka ilipwe na sio kumzuia Kessy asicheze Yanga

No comments: