ASYA IDAROUS KUWAKILISHA TANZANIA KATIKA AFRICAN FASHION WEEK BOSTON

 Mama wa Mitindo Asya Idarous kuwakilisha Tanzania katika African Fashion Week, Boston
Mama wa Mitindo Mkongwe anayefanya vizuri ndani ya Tanzania na Nchini Marekani, Asya Idarous Khamsini  jumamosi  ya Novemba 26.2016 anatarajia kuwakilisha Tanzania katika usiku maalum wa African fashion Week Boston, Marekani.

Jukwaa hilo maalum la mitindo limeandaliwa na House of Nadhra Boston USA,  huku mbali na Mama wa Mitindo Asya Idarous, pia litajumuisha Madesigner kutoka  kona za Afrika, Ulaya na kwingineko.

Tukio linatarajia kuwa na watu mbalimbali watakaojumuika pamoja kushuhudia mavazi ya ubunifu  hasa kwa ubunifu wa hali ya juu kutoka kwa wabunifu wa Afrika. Pia mbali na jukwaa hilo la mitindo pia kutakuwa na muziki wa ‘Live band’.  Vyakula maalum vya kiafrika,  pamoja na uuzwaji wa bidhaa za kiafrika.

Eneo la tukio hilo: Hibernia Hall, Boston, MA


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.