WATUHUMIWA 05 WAKAMATWA NA POMBE BANDIA AINA YA KONYAGI NA VIFAA VYA KUTENGENEZEA KINYWAJI HICHOJeshi la Polisi kanda maalumu Dar es salaam linaendelea na oparesheni mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya jiji na kufanikiwa kukamata watuhumiwa jumla ya watuhumiwa  67 kati yao watuhumiwa watano walikamatwa kwa makosa ya kuuza na kusambaza pombe bandia aina ya konyagi na vifaa vya kutengenezea kinywaji hicho kama ifuatavyo;


1.Chupa tupu za konyagi 175.(2.) Chupa zenye kinywaji cha konyagi 17. (3.) Vifungashio vya viroba vya konyagi 111. (4.) Vifuniko vya  chupa za konyagi 200. (5.) Lebo na stika za konyagi.(6.) Katoni 111 za viroba vya konyagi. (7.) Vimiminika vya pombe aina ya spiriti lita 20. (8.) Ndoo kubwa aina ya jaba moja na koki 10 .(9.) Viroba original pakiti 14,916 (10.)Victorious pakiti 1,080.

Watuhumiwa waliokamatwa na bidhaa hizo bandia ni kama ifuatavyo;
1.LADNESS GRATION KAGARUKI miaka 26, mkazi wa sinza madukani

2.ALOYCE EMMANUEL miaka 53, mkazi wa Salasala
3.LEORNAD AROBOGASTI miaka 49, mkazi wa Makongo.
4.GODFREY GABRIEL miaka 29, mkazi wa Mwenge.

5.AVELINE SANDOLE miaka 58, mkazi wa Mwenge.
Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Habari Nyingine Kutoka Polisi zipo chini-----------

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WAWILI WA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU

Tarehe 20/11/2016 saa 09.00 jioni huko kariakoo mtaa wa mkunguni na sukuma Polisi ilipokea taarifa toka kwa SAHIM MOHAMED (24),  kwamba meneja masoko wa kampuni ya DISCOUNT CENTRE akiwa nyumbani kwake jengo la ghorofa 07, alivamiwa na watu wawili wakiwa na silaha za jadi.
Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kuwawahi watuhumiwa  RAMADHANI ABDI (42) mkazi wa jangwani na AMIRI ALLY (50), mkazi wa Tabata. Watuhumiwa walikamatwa na vifaa mbalimbali walivyoiba kabla hawajaondoka eneo la tukio na vifaa hivyo ni laptop 01, ipad 01, pesa taslim Tsh 120,000/= na silaha  walizotumia kuiba ni visu, bisibisi na kipande cha nondo.
 watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika watapelekwa mahakamani.
POLISI KANDA MAALUM DSM WAMEKUSANYA TSH 414,060, 000 /= KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi Kanda maalum DSM kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 17.11.2016 hadi tarehe 21.11.2016 na kuingizia serikali mapato ya ndani kama ifuatavyo;

1.     Idadi ya magari yaliyokamatwa                             - 12,923
2.    Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa                              - 879
3.    Daladala zilizokamatwa                                        - 3,163
4.    Magari mengine (binafsi na malori)                         - 9,760
5.    Bodaboda waliofikishwa Mahakamani                         -
kwa makosa ya kutovaa helmet na
kupakia mishkaki                                                            -
6.    Jumla ya Makosa yaliyokamatwa                           -  13,802

Jumla ya Fedha za Tozo zilizopatikana    Tzs 414,060,000/=.
 
Madereva wote wanatakiwa kutii sheria za usalama barabarani na washirikiane na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani ili kudhibiti matukio ya ajali zinazoweza kuzuilika.SIMON N SIRRO- CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.