POLISI WAOKOA BASTOLA MOJA, SIMU NA MALI ZILIZOIBIWATarehe 17.11.2016 saa 03:15 asubuhi huko maeneo ya maduka mawili Chang’ombe. Polisi walifanikiwa kuokoa silaha aina ya bastola GLOCK 19 yenye no. ELS377 Ikiwa na risasi 17 pamoja, mabegi matatu ya nguo na simu tano.

Mafanikio hayo yalipatikana mara baada ya Polisi kupata taarifa kwa raia mwema kwamba kuna kundi la vibaka walienda nyumbani kwa KIM DAVID MGAYA na kugonga na kujifanya wana mzigo wa bosi, na baada ya kufunguliwa waliingia kwa mfululizo vibaka zaidi ya 13 na kuwaweka chini ya ulinzi wanafamilia waliokuwepo ndani na kuwafunga kamba mikononi, miguuni na plasta mdomoni na kuendelea kupora.


 Baada ya askari kufika eneo la tukio haraka waliwakuta vibaka hao wakiwa wanatoka katika nyumba hiyo na mabegi walipowaona Polisi walitupa mabegi na kuanza kukimbia kwa miguu na kutupa mabegi hayo ambapo ndani yake kuna Bastola aina ya GLOCK 19, simu za mkononi za aina mbalimbali na vitu vingine. Ufuatiliaji na Upelelezi wa kuwatafuta vibaka hao bado unaendelea na raia wema waendelee kutupa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhakika za kukamatwa kwa watuhumiwa.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.