Mkali wa Wowowo Zaiid akitoa Burudani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Songea.
Likiwa limeingia mkoa wanne
Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote limefana na kuacha alama kwenye uwanja wa
Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma
usiku wa kuamkia jana, Kabla ya kuingia mkoani humo Tamasha hilo lililoanzia
Mkoa wa Morogoro limepita mikoa ya
Rukwa, Iringa, Songea na kuelekea Mtwara jumapili hii.
Akifungua Tamasha hilo Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme aliyeongozana na mkuu wa wilaya ya Songea
Mjini Mhe. Pololite Mgema alisema
Tunawashukuru Kampuni ya Tigo na Clouds Media kwa kutuletea tamasha hili kubwa
mkoani kwetu. “ Hii si kwa burudani pekee bali ni fursa kwa wakaazi wa mkoa huu
kwa kuwawezesha kwa kuwaongezea kipato kwa kipindi hiki chote cha wiki nzima”.
Niendelee kuwapongeza tena Tigo na
Clouds Media na kuwaomba mwakani msiache kuja tena kwenye mkoa wetu.
Kwa upande wa burudani, ilianza
kwa kumpata mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Supa Nyota kwa
kumuibua Msanii Single Baba atakayeiwakilisha Ruvuma kwenye fainali
zitakazofanyika jijini Dar Es Salaam mwezi ujao.
Shoo rasmi ilianza kwa Msanii
Mesen Selekta kufuatiwa na Rubby huyu ni msanii aliyeibuliwa kwenye Supa Nyota
miaka kadhaa iliyopita, kwa kweli ni msanii wa aina yake aliweza kuteka hisia za
mashabiki kwa kuimba nyimbo tofauti tofauti zikiwemo Niwaze,Ntade, Na
Yule,Forever na nyingine.
Jumla ya wasanii kumi na mbili
walipanda jukwaani wakiwemo Rostam, Weusi, Ruby, Mr. Blue, Barnaba, Zayd, Fid
Q, Masen Selekta, Lulu Diva,Chege, Foby
ambao wasanii hao ndio watapanda kwenye jukwaa jumapili uwanja wa Nangw’anda
Mtwara.
Mdhamini mkuu wa msimu huu,
kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Sumbawanga
kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kama Lote
inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia
menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu
huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa la
bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo
Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo
Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa
watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua
namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta
78888888.
Wateja wa Tigo pia watapata faida
zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa
zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu
janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono
la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno
MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya
http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la
muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu
linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo;
Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba,
Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es
Salaam.
|
No comments:
Post a Comment